Leo kulikuwa na kikao maalum cha wanawake kilichoitishwa kwa ajili ya kuzungumzia maendeleo ya wanawake Tanzania. Kikao hicho, kilihusisha Wataalamu toka Wizara yetu ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum pamoja na viongozi wote wanawake chini ya TWCC. Tunamshukuru sana Mwenyekiti wa “Tanzania Women Chambers Of Commerce” kwa kuitisha kikao hicho adhimu kwa ajili ya maendeleo ya wanawake wote. Kinachofurahisha ni namna kikao hicho kilivyobeba wanawake viongozi wa taasisi mbalimbali kutoka mkoa wa Dar Es Saam na mazungumzo yalijikita ni namna gani tunaweza kumasaidi Mhe Mama Samia Suluhu Hassan, Raisi wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika kumjenga mwanake kulingana na mapendekezo ya Beijgin ya Gender Equality . Katika kuchangia mada mbalimbali ndipo michango yetu na namna tulivyokuwa na mijadala mitamu mara ikazaliwa dhana ya ‘High level Women’.
Kama kwa mara ya kwanza ndio umejaliwa kutembelea ukurasa huu, nipende tu kukujulisha kwamba ,ukurasa huu wa wanawake unalenga katika kupeana na kuwapa taarifa za wanawake wa Tanzania katika lugha nyepesi sana ili TWENDE na MAMA!. Sasa hili neno la “high level Women” na hiki kidhungu inahusu kweli? ha ha ha ha! Unajua kujitambua ni jambo muhimu sana katika maisha yetu. Kupitia kikao chatu kuliibuliwa neno…”High level Women” hii ikiwa na maana kwamba, tumeamua wanawake wa Tanzania kuwa sura za viwango vya kimataifa sasa! Kwani kuna shida? Wanawake wa Ushirika wa viwanda vya wanawake vya MADIRISHA pia tulihudhuria. Na mnajua ninavyo upigia USHIRIKA DEBE kwa wanawake hapa nchini na Afrika nzima. MADIRISHA tulihusishwa tukiwa na wadau wengi wengine ambao sitaweza kuwataja wote, kwa sababu ya nafasi lakini ni kiri walikuwemo akina mama nguli kweli kweli yaani wanawake wa matokeo makubwa ambao kwa uchache wao ni akina Hilda Kitonka, Maida Waziri, Mercy Mchechu, Mwanjuma Hamza, Anna Matinde, Mhe Sophia Simba kiongozi wetu kuntu bila kumsahau mama la mama Mhe Mama Mercy Silla nk.
Kikao cha leo kililenga kutoa maoni na mambo mbalimbali ya maendeleo ya wanawake nchini, na kweli ukumbi ulizizima kwa furaha na matumaini mapya ambayo yalilenga katika kumjenga mwanamke wa Tanzania. Tumejifunza kwamba wanawake sasa tuanze kuongea lugha kubwa! Mipango mikubwa mikubwa! Kikubwa ni kuendelea kujituma sana na kuwa na malengo ya kimkakati. Wizara yetu ya maendeleo ya jamii iko kazini na sisi wanawake tuwe kazini. Yaani tuwe watu wa “High level”.. kabisaa! Kwani ni nani katukataza?
Michango mingi ililenga katika kuonesha namna gani wanawake wanaofanya, kazi kubwa ya kutambua wanawake waweze kutambuliwa ikitokana na michango ya kundi namba mbili mada ambao katika mazingira ya mijadala yetu zilichangiwa na Mama Suzy Laiser na Anna Matinde. Imefika hatua wale wanawake ambao wanatoa michango katika maendeleo ya wanawake watambuliwe. Ni dhahiri kwamba, wanawake ambao wamejenga wanawake wengine ifike hatua Watambuliwe na mihimili muhimu! Katika kuchagia mada hiyo Mama Anna Mantinde ndiye alionesha hali ya kuchoshwa na kazi kubwa aliyoifanya kwa wanawake na hata mjumbe mmoja Maida Waziri naye alisisitiza juu ya kazi kubwa ambayo wanawake wamefanya. Kikubwa inabaki kuwa changamoto kubwa kwa waandaji wa mjadala huo katika kufanyia kazi maoni yaliyotolewa.
Mwisho kabisa ningependa kusema kwamba, kwa maoni yangu wanawake wote wa Tanzania, tujiamini kwamba ni wa viwango vya kimataifa kwa kazi kubwa tunazofanya toka Majumbani hadi Masokoni na Makazini. Kila mmoja ajiamini kwa mchango anaoutoa katika kujenga jamii zetu. Hakika tumeweza na sisi wote ni High Level Women. Kikubwa kumekucha Tanzania na Jogoo keshawika Mama yetu anaupiga mwingi, sisi akina mama ndio wakucheza ngoma ili chakula kisipoe. Kumekucha wanawake wenzangu. Mdau wenu Fatma Kange napenda kuandika na nitaandika habari zenu bila choyo kwa kadiri Mwenyezi Mungu atakavyonijalia, kama sehemu ya kuunga mkono kazi ya Mhe Raisi na mambo mazuri aliyotuandalia hadi kutuletea Wizara. Hivi tupewe nini wanawake?. NAWAPENDA SANA WANAWAKE WA TANZANIA. Kazi ziendelee!
Wanawake wa Tanzanai sasa kuchelee!
Wanawake wa Afrika walihitaji ushirika.

It ia good
Asante kwa kujali unaweza kuwatumia watu mbalimbali wanawake waweze ku subscribe kwa makala zangu za wanawake
Ilikuwa ni team kabambe aka ‘think tanks’
Nice article Fatma, 👏🏽 keep up the good job
Asante sana Irene Makini kwa kujali na kukomment. Kwa kweli ni Team Nzuri mno na tuendelee kupiga kazi!
Wow! Breath taking article. I love reading.
Congratulations Fatma.
Thank you so much my Dear.
Mrs Mercy Silla.
Thank you so much Madam Chair
Tanzania Women Chambers Of Commerce (TWCC)
We are here to support you big time MAMA.
As women of Tanzania we need each other and its time we work together.
We call it helping Hand between each one of us!
Thank you for a good work.
Barikiwa,
Be blessed more.
Safi sana Fatma. Keep it up.
My sister Tatu Jongo
Thank you for your message
Karibu Sana Dear.
Shukran Fatma kwa makala nzuri nikiwa mmoja wa wamama wa high Level nasema tutafika pale tulipo dhamiria
Salma Seif
Asante sana kwa kuukubali U high level. Inshallah kikubwa kujitambua na kukubaliana kuanza kufanya mambo makubwa
It can be done
Hongera.
This is so amazing. We really connected and had a productive day.
Madam Vanancia Msita
It was such a beautiful moments
We need a lot of such activities in Tanzania
Something like women connect etc
Thank you very much for your message.
We enjoyed the whole moments of the dialogue it was at the Higher Level for real, we are looking forward for the upcoming results of the United Nations Development Programs in their Sustainable Development Programs for what we have chosen, Equality
Asante kwa makala hii
You are welcome madam Jamila Rajab Assakheir
Thank you for ur time you took to read my Makala and comments.
Find a day you come for interview madam Anzia Sokoni. Ahsante sana.