TWEA AFRICA

TWEA- INAKUKARIBISHA KWENYE-MAFUNZO YA WANAWAKE NA UONGOZI WA USIMAMIZI WA MAKAMPUNI -WANAZOENDESHA- TAREHE 30.06.2022.

TWEA tumejikita katika kutoa kozi maalum ya Uongozi wa Kitaasisi. Unajua toka harakati za kumkomboa mwanamke zimeanza nchini na duniani kote akina mama wamekuwa watu wakuchangamkia fursa. Wengi wameishia kufungua kampuni zao. Kikubwa kinachofanyika sasa kupitia TWEA AFRICA-ni kufundisha uongozi wa kuendesha taasisi zao. Kuwa na kampuni ni mzigo mwengine tumejitishwa yataka mbinu sahihi za kuundesha ili ukae sawa, na matokeo upate. Usitwange maji kwenye kinu!

Nimechukuwa uzoefu wangu wote wa kuendesha taasisi ya GS1 Tanzania kwa miaka 10 katika kozi ya siku mmoja, yaani nakupitisha kwenye njia zote nilzotumia kusimamaisha huduma ya Barcodes nchini kwa ufanisi mkubwa. Ni kama natoa siri ya mafanikio. Na unawezaje ku balance kati ya Kazi zako, Maisha ya Familia na Uongozi. Kwa kweli hadi vitabu nilivyosoma kunijenga, Makala zangu na mbinu za kuendesha taasisi katika mazingira ya Tanzania ninaweza kutoa kupitia mafunzo hayo.

Leo ukiniuliza kuhusu safari yangu ya kikazi, uongozi na umama, nilivyoweza ku balance ujue kabisa kuna mambo mengine lazima katika kujipanga unaachana nayo. Muda kupanga na matumizi yake ambayo utakuwa nafasi ya kubalance Nyumbani na Kazini na kote ukawa na matokeo makubwa ndicho hasa kilichonisukuma kuanzisha hili somo la UONGOZI WA WANAWAKE WENYE MAKAMPUNI NA NGO. Nina miaka 10 ya uongozi wa Taasisi nikiwa ni mwenye mambo mengi na huku nikianzisha miradi mikubwa. Zipo mbinu za kufanya ambazo darasa hili ni maalumu kwako wewe kiongozi wa kampuni yako. Uanaweza kuniandika ili kushiriki katika mafunzo hayo.

Tanzania sasa kuchelee

Wanawake wa Africa walihitaji zaidi USHIRIKA.

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *