Tabia za kupunguza ili kuwa na mali au Fedha kwa wanawake

Kuna vitu hata mimi navitamani ningevijua nikiwa na miaka 17 hivi! Misingi ya maisha na fedha. Ni kama elimu hii ni muhimu kama somo la Biologia mmh! Kwani hutoa misingi ya maisha yetu ya dunia na utajiri-au Fedha. Naamini vitabu vinasehemu kubwa sana ya kumtengeneza mtu katika muogozo fulani. Leo katika makala yangu hii nimejikita kidogo kwenye namna wanawake tunavyoweza kuacha au kupunguza mambo fulani kwa ajili ya kuwa na akiba ya kutosha au kuwa na fedha kama sio Utajiri. Kuwa na fedha au akiba kubwa ni sayansi kabisa! Haiji hivi hivi labda umeibiwa siri.

Yapo makabila nchini Tanzania ambayo utafutaji ni sehemu yao ya kitamaduni na kuhifadhi hela ndio maisha yao ya kila siku, inategemea misingi yako ni ipi, lakini wapo watu wengine elimu ya kuhifadhi pesa tunatakiwa kabisa tujifundishe, wala hujachelewa.

Wanawake sisi kwa kweli ni mabingwa wa matumizi,mengi mengi, lakini sio mbaya tunaweza kujifunza hatua tano muhimu za kubana matumizi na kuwa na akiba ya kutosha nikumnukuu Adam wa Wealth Builder. Yeye anasisitiza mambo yafuatayo.

Hatua ya Kwanza “Kupunguza Matumizi Makubwa”. Huwezi kutumia zaidi ya unachoingiza. Yaani wewe unatumia tu bila kujikagua hivi ninangiza shilingi ngapi. Matokeo yake unafanya matumizi bila kutathmini kipato chako kama mtu asiyetafakari mambo. Kuanzia sasa chukua kalamu yako na karatasi utafute chanzo chako cha pesa na ujue matumizi yako, utajilaumu.

Kipato kitaongezeka tu endapo utapunguza matumizi yako ya leo. Hebu kagua pesa zako zinapokwenda na uone njia sahihi ya kulinda fedha zako.

Hatua ya Pili ‘Tumia fomula ya 80/20’Badilisha matumizi yako kwa kutumia hii fomula. Hili la asilimia 80 kwa 20 lina maana kwamba. Kila kipato chako unachokipa chukua asilimia 80 kwa ajili ya matumizi na asilimia 20 kwa ajili ya akiba. Utafanikiwa zaidi kama utachukua katika akiba yako ya asilimia 20 ukaigawa kwenye makundi yafuatavyo, Gawa kwa -MAD- yaani Mtaji, Akiba na Dharura. Fanya hivyo kwa muda mrefu na nakuahidi utaiona tofauti.

Hatua nao Tatu “Jimaarishe kwa Maarifa”-Self improvement. Hii ina maana kwamba kuacha kujiimarisha kwa marifa ni dhuluma sana mwanamke unajipatia wewe mwenyewe kwa kutotauta ujuzi au elimu. Bila Elimu au ujuzi wa kujiongeza kila mara, utakwama! Nakuuliza ni lini mara yako ya mwisho umesoma kitabu? au umekwenda seminar au washa ya kujisomea jambo? Au umelipia kusoma jambo lolote? Haya yote kama hujiendelezi ni dhahiri itakuzuia katika kujifunza jambo jipya na kukuongezea akiba na kipato kikubwa.

Hatua ya Nne “Jiwekee Malengo ya Kifedha” Kutojiwekea malengo ya kifedha ni kujichelewesha. Jitathmini leo upo wapi sasa, kwenye kipato chako na unataka kuwa na kipato gani baada ya muda gani. Kila kitu ni kujifunza, jipime na tafuta mbinu zote zitakazokufanya uwe na kipato halali bila stress kubwa. WEKEZA!

Hatua namba Tano “Jifunze kuhusu masoko ya Mitaji ya Kifedha”. UTT taasisi ya serikali inatoa elimu kubwa na ina mifuko kadhaa kwa ajili ya uwekezaji katika mitaji ya fedha. Ni wakati sasa kwa wanawake waweze kufuatila taratibu hizo za mitaji ya masoko na kuwekeza.

Tanzania sasa kuchelee.

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *