Ziara ya viongozi wa Madirisha - Industrial Park

VIWANDA VYA USHIRIKA WA WANAWAKE WA VIWANDA KUJENGWA

Mwenyekiti wa Ushirika wa viwanda na ushirika vya wanawake pamoja na wanachama wake wote wameonesha nia yao kubwa kuona viwanda vichache vinaweza kujengwa. Bidhaa za ushirika wa madirisha zimeanza kujitokeza katika sekta mbalimbali za ushirika wanazo shiriki kama Batiki, Asali, Mlonge, Mchele, Maharage, Samaki, Shanga na Urembo nk. Maushirika haya yanalenga katika kujenga nafasi ya mwanamke katika kushiriki uchumi wa viwanda kiushirika. Katika kuhakikisha hilo linawezekana Chama cha Ushirika wa VIwanda vya Wanawake pamoja na viongozi wa chama hicho, na kwa kushirikiana kwa karibu na serikali kupitia Tume ya Ushirika waweka misingi imara ya chama na viwanda vyake.

Ushirika huu wa viwanda vya wanawake kwa njia ya Ushirika wa MADIRISHA- wameanza ziara za kutembelea maeneo mbalimbali ambayo wanaweza kuweka viwanda vyao. Safari hii walifanya ziara ya viwanda katika eneo la Mlandizi lilipo Kibaha kwa ajili ya kupata uelewa wa kina juu ya Industria Parke na namna itakavyoweza kuhakikisha ushirika huu unavyomiliki viwanda vyake.

Pichani, baadhi ya viongozi wa Ushirika wa MADIRISHA katika picha katika eneo la viwanda Mlandizi Mkoa wa Pwani. Tunampongeza Mwenyekiti wa Ushirika huo, pamoja na Board nzima kwa kazi kubwa sana wanayoendelea kuifanya. Wanawake nchini Tanzania Kuchelee!

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *