Waafrika ni taifa kubwa sana duniani lenye tamaduni zake. Katika mambo mengi ambayo huwaunganisha waafirika ni Uoto wa Asili, na neema kubwa sana ya ardhi yenye rutuba katika kila eneo la bara hili. Hata hivyo ipo alama ambayo ni kama bendera ya waafrika mahali popote duniani wanapozungumziwa. Alama hiyo ni urembo wa Shanga ambao kwa kiasi kikubwa ni sehemu ya utambulisho wa asili yetu, na bara letu. Tanzania kama ilivyo nchi nyingine za bara la africa makabila yake mengi yamegubikwa na utamaduni wa shanga.
Ushirika wa Viwanda vya Wanawake vinavyojulikana kama MADIRISHA umeona kwa dhati kwamba katika kujenga uelewa mpana wa tunu hii ya shanga, inabdidi kuwasaidia akina mama waliopo kwenye Industry ya Urembo wa Shanga kuunganisha nguvu na kuzalisha shanga bora zenye muonekano wa Made in Tanzania. Wengi wa akina mama ambao hushiriki katika biashara ya shanga na urembo wanakiri kwamba sanaa ya Shanga na Urembo ni ajilra kubwa, ni kipato na tumaini la familia zao kimaslahi.
Mwenyekiti wa Ushirika huu Bi Marium Abdallah Ally amenihakikisha kwamba, si tu kwamba anataka kubadili sura ya shanga tanzania bali kuifanyia mapinduzi makubwa ili iwe kama biashara zingine kubwa nchini na duniani kwa ujumla. Tunamuombea azidi kupata maono makubwa katika kujenga Ushirika huo wa Shanga na urembo nchini.
Shanga ni Mali, Shanga ni Biashara, Shaga ni Furssa!
Kama unataka kushiriki katika ushirika huu wa wauza shanga, watengenza urembo wa shanga, mikufu nk tafadhali tembelea ofisi zetu zilizopo Tegeta Jijini Dar Es Salaam.
