Mkoa wa Dar Es Salaam umejizatiti katika kujenga kizazi kipya cha wanawake wazalishaji ambao watazalisha kwa Ushirika. Kikao kazi kilichofanyika havi karibuni kiliazimia mambo mengi ya msingi na kukubaliana kwamba ushirika ndio nguvu ya mnyonge. Viongozi wote wanaosimamia jitihada mbalimbali za maendeleo ya wanawake mkoa wa DSM walishirikishwa katika kikoa hicho. Tumefarijika kwa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa kuitisha kikao hicho, na kuomba ushirika wa Viwanda vya Wanawake vya MADIRISHA kufanya uwasilishaji.– Presentation.
Baada ya uwasilishaji wetu, umeonekana kwamba Mkoa wa Dar Es Salaam utahamasisha masuala ya ushirika kwa wanawake. Tunawapongeza sana, sekretariate ya Mkoa wa DSM kwani jukwaa la wanawake mkoa wa Dar es Salaam chini ya Uratibu wa Dr Elizabeth Mshote na Uongozi wa Mkuu wa Mkoa wa Dar Es Salaam, Mhe. Amos Makalla, limeweza kuonesha mafanikio kadhaa ikiwemo kuandaa mafunzo mbalimbali ya uwezeshaji kwa wanawake mkoa wa DSM. Katika kuhakikisha kwamba, mambo yote yanayohusu wanawake wa mkoa wa Dar Es Salaam yanaratibiwa vizuri, ofisi ya mkuu wa mkoa imeahidi kusimamia utekelezaji wa maazimo mbalimbali ambayo yaliamuliwa katika kikao hicho. Wanawake Mkoa wa DSM Kazi Zinaendelea!!. Pichani- Mhe Mkuu wa Mkoa Amosi Makala akitoa maelekezo kwa viongozi jukwaa la wanawake mkoa wa Dar Es Salaam katika kikao hicho.
