Mkurugenzi wa Masoko wa UTT ndugu Daudi Mbaga ameonesha nia yake ya kuwajengea uwezo wanawake wa Ushirika wa viwanda vya wanawe na kuona namna watakavyotumia fursa hiyo katika kumjengea kila mwanamke uwezo ili kupata mitaji endelevu. Mfuko wa UTT unalenga kuhusisha masuala ya kifedha ili kuweza kuwafikia makundi yote nchini, hususani ya akina mama. katika kuziona fursa zilizopo katika sekta ya kifedha. Wanawake wengi bado hawajaweza kutumia fursa hiyo vizuri hapa nchini.
UTT imekua ikifanya makongamano mengi ya kuelimisha marika na sekta mbalimbali ili ziweze kufahamika kwa manufaa ya wanachi wote kwa ujumla hususani Wanawake na Vijana. Akiongea kutoka Morogoro Ndugu Daudi Mbaga amesisitiza kwamba, katika kuhakikisha kwamba elimu ya uwekezaji wa kifedha inawafikia wanawake UTT inataka kuongeza nguvu kwa wanawake wana- Viwanda Nchini.
Mwaka huu chama cha Ushirika wa viwanda vya wanawake kimepanga kufanya makongamano kadhaa ambayo inategemea kufanya kazi kwa karibu na UTT ambao wameonesha nia ya kumjengea uwezo mwanamke kwa kitanzania katika kutimiza malengo yake.
Wanawake wa Tanzania sasa kucheleee!
