Chama cha Ushirika wa Viwanda cha Wanawake cha MADIRISHA, kimekuwa na wakati mzuri katika kongamano la pili la utafiti wa ushirika uliomalizika leo mkoani Dodoma. Akiripoti kutoka kwenye kongamano hilo, Afisa habari wa MADIRISHA Bi Anna Mary Leone Kavishe anasema kwamba, nafasi waliyopewa ushirika huo, katika mkutano huo ulikuwa ni wa kipekee na wenye kutia moyo sana. Ametoa ushauri kwa wanachama wa MADIRISHA kuzidi kushikama katika kujenga chama hiki kipya cha ushirika wa viwanda vya wanawake nchini.
Jumla ya watu 600 wameshiriki katika kongamano hilo ambalo limehudhuriwa na naibu Waziri wa Kilimo ndugu, Antony Mavunde. Kaika hutuba yake Mhe Mavunde amesisitiza kwamba , “Vyama Vya Ushirika viwekeze katika kujenga Utajiri na sio Migogoro” na vizingatie Sheria, Uongozi Bora, Uwajibikaji na Uadilifu. Amesema kanuni za Ushirika ziheshimiwe katika kusimamia vyama vya ushirika nchini.
Chama cha Ushirika cha wanawake kimeweza kutoa salam za shukrani kwa niaba ya wahudhuriaji wote wa kongamano hilo ikiwa ni sehemu muhimu na kubwa sana kwa chama hicho kipya nchini. Bi Monica Mlowezi ameweza kutoa salamu hizo kwa niaba ya vyama vyote vya ushirika vilivyohudhuria kongamano hilo.. Bibi Monika anawakilisha kiwanda cha ushirika cha bidhaa za Mlonge, chini ya uwenyekiti wa Bi Asia Msusa. Takribani vyama 200 vya ushirika viliweza kuhudhuria konngamano hilo
Chama cha Ushirika wa Viwanda vya wanawake nchini kinashukuru Tume ya Ushirika na kipo tayari kufanya kazi kubwa ya kuleta mabadiliko kwa kuzalisha bidhaa zenye hadhi za kimataifa ikizingatiwa ni chama cha wanawake. Tume ya Ushirika itegemee makubwa kutoka chama hiki chenye wanawake walioamua kujipanga upya kiviwanda.
Wanawake wa Tanzania sasa Kucheleee!
