Watu wanazidi kupata uelewa na maendeleo hayapigi hodi, maendeleo huchochewa zaidi na hatua jamii inayopiga kila mara. Mwaka huu TWEA ikiangazia kuhusu wanawake vinara wanaofanya mambo tofauti na ya kimaendeleo inakutana na mwana dada lidhtiness ambaye ameona ipo haja ya kuanzisha tuzo maalumu za kuwatambulisha SMEs wanaothubutu pamoja na taasisi zinachochea maendeleo ya SMEs hao.
Mkoa wa Mwanza umepata baraka kubwa kwa tuzo za JASIRI AWARD kuweza kwa mara ya kwanza kufanyika katika mkoa huo wenye shughuli nyingi za kiuchumi. Tuzo hizi kufanyika kwa Mkoa wa Mwanza kunazidi kufungua pazia la kuunganisha jitihada za serikali katika kuweka mazingira bora na wezeshi katika kujenga biashara na kutambuliwa kwa sekta binafsi inayojipanga na kukua.
Watu walioshirikishwa ni katika vigezo mbalimbali ambavyo vimeshindanishwa kwa muda wa miezi takriban mitatu ili kupata washindi wa tuzo hizo za Mkoa wa Mwanza zinazojulikana kama JASIRI AWARDS 2022. Vigezo viliweza kuwaleta washindi ambao mara hii hawakutokea tu mkoa wa Mwanza lakini pia katika mikoa mbalimbali nchini. Mkuu wa mkoa wa Mwanza ndiye amekuwa mgeni rasmi katika tuzo hizo zilizofana sana.
Mwasisi wa Tuzo hizo Bi Lightness Nkamba Budodi amesema kwamba tuzo za mwaka huu zimefanikiwa sana na atafanya vizuri zaidi kadiri miaka inavyokwenda
