Nchi ya Benin na Ugali Nyama

MAKALA YA COTONOU, BENIN NA RAMADHANI NGODA wa Azam Sport.

Kila nchi ina utamaduni wake. Nimebahatika sana leo kukutana na makala ya michezo ya AZAM Sport. ikiangazia taarifa za soka kutoka nchi ya Benin. Jambo lililonivutia ni utangulizi wa makala yenyewe. Utangulizi wa makala hizi ambazo zimetanguliwa na utamaduni wa chakula na watu wa Benini ulikuwa mzuri mno na wakuvutia. Kilichonifurahisha zaidi pia ni kuona vijana kutoka mikoa ya kusini wanatafuta maisha katika nchi ya Benini wakageuka kuwa ni wafasiri katika makala hiyo nzuri ya Azam ya michezo. Maisha ni kujiongeza hongereni sana watanzania nyie ambao majina yenu nilishindwa kuyanukuu vizuri. . Ramadhani Ngoda anasema usafiri wa boda boda unachukua sehemu kubwa ya usafiri nchini Benin kama ilivyo nchini Tanzania..

Nimeona katika kipindi hicho cha Azam vijana hao wa kitanzania wakimsaidia mtangazaji Shabani Ngoda kufasiri aina za vyakula vinavyoliwa nchini Benin. Nimejifunza ule usemi wa Marehemu baba wa Taifa Mwl Nyerere aliokuwa akisema AFRIKA NI MMOJA! Chakula kikuu nilichokiona katika makala hiyo ni Ugali wa Mahindi, Ugali wa Mhogo, Nyama ya Ngombe, Samaki na Mboga za majani zilizowekwa karanga. Wakati wanamalizia ile makala wanasema chakula nchini Benini hakina matabaka uwe tajiri au masikini hicho ndio chakula utakachokuta kinauzwa na kuliwa na kila mtu karibia kila mahali, TEMBEA UONE!

Hongera sana Azam naamini kupitia makala hizo wanawake wa Tanzania tuna nafasi kubwa ya kujifunza ulaji wa vyakula na fursa za nchi mbalimbali kutoka barani Africa. Makala ya leo ni nzuri mno na ukurasa huu wa TWEA umelenga katika kuhakikisha fursa za kiuchumi zinatafsiriwa kwa lugha nyepesi kwa ajili ya Soko la Africa linalotusubiri wanawake wa Tanzania!

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *