Taasisi ya uwezeshaji wananchi kiuchumi NEEC imeandaa maonesho ya mifuko ya Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi nchini ya tano. Kupitia maonesho hayo taasisi ya GS1 Tanzania nayo imealikwa kushiriki. Ushiriki wa GS1 Tanzania katika maonesho hayo unatija kubwa sana sio tu kwa viwanda pekee bali kwa wazalishaji wanawake wa Mkoa wa Morogoro ambao wanaweza kupata huduma ya Barcode kiurahisi katika maonesho yanayoendelea.
Taasisi ya GS1 Tanzania inaipongeza sana NEEC kwa kazi nzuri inayoendelea kuifanya kwa manufaa ya wananchi nchini. Taarifa za mifuko hiyo zitatoa nafuu kubwa kwa watu mbalimbali kujipanga kwa ajili ya kuzitumia fursa zilizopo kupitia mifuko ya uwezeshaji nchini. Kuhusishwa kwa GS1 Tanzania kwenye maonesho hayo pamoja na wadau wengine kunazidi kuipa umuhimu taasisi hii iliyojikita katika maendeleo ya viwanda nchini hasa kuchangia na kuchochea ukuaji wa jitihada za wanawake, katika maendeleo ya ujasiriamali tunayoyaona hapa nchini, wanawake wengi wanajihusisha na biashara kubwa ya usindikaji, hivyo huduma za barcodes ni muhimu katika kujenga uchumi wa viwanda vya wanawake.
GS1 Tanzania katika maonesho hayo imewakilishwa na mtaalamu wa barcodes wa vikundi, Ndugu Erick Kafula ambaye hufanya kazi kubwa katika kuwafikia wazalishaji wanawake nchi nzima. Wanawake mkoani Morogoro huu ndio muda muhimu sana wa kushiriki katika maonesho hayo na kupata huduma za barcodes, kwa wakati ambapo maonesho hayo yanaendelea.
GS1 Tanzania inaipongeza sana NEEC kwani kwa miaka 10 ya ufanyanji kazi wake wamekuwa ni wabia muhimu katika maendeleo ya Barcodes nchini. Katika maonesho hayo, taasisi mbalimbali zimeshiriki sambamba na GS1 Tanzania na hivyo itazidi kuwapa fursa wadau wa viwanda hasa wanawake katika kujipanga na uchumi.
Wanawake wa Tanzania sasa kucheleee!
