Leo katika segment ya ISHI Happniess for women, nimetohoa motivation quote mmoja mtandaoni ikisema ” A happy life doen.t just find you, you make it yourself” hii motivation imeandikwa na ‘”Success Minded”. Na kama unavyofahamu ukurasa huu wa TWEA umejikita kwa wanawake na mambo yao, na vile tuna segment ya ISHI ambayo inahamasisha FURAHA kwa wanawake makala hii naiandika.
Ni dhahiri kwamba wanawake waliowengi utakuta ukiongea nao kila saa analaumu jambo fulani, linalomkosesha furaha yake. Wanawake wamekuwa ni watu wa kusononeka sana. Jambo hilo sio zuri kabisa na mara nyingi mwanamke mwengine anaweza kulalamikia watoto, ndugu, majirani, ofisi, mume au watu mbalimbali. Kikubwa ambacho wanawake wanatakiwa kukijua na hii nasema baada ya kupata mafunzo mengi sana kwenye maisha. Furaha yako haimtegemei mtu, lazima uwe na uwezo wa kujipanga kupata furaha. Wengi walifikiria furaha zinatokana na watu, au nje yako. Kwa ujumla maisha ya furaha yapo mikononi mwako. Wewe ndiye mwenye hatima kubwa katika kujipangia furaha na aina yake.
Timiza wajibu wako, kila idara unayotakiwa kutimiza wajibu timiza, ukimaliza jitafute wewe mwenyewe, sehemu yako ya kulala, sehemu yako ya kulia chakula, sehemu yako ya wageni na mzunguko wa nyumba unayoishi hata kama ni ya kupanga, hakikisha inakupa tabasamu. Weka mazingira yako ili yafanane nakile unachotaka kukiona kikikutibu furaha yako. Mwengine unamkuta anakaa nyumba hapigi rangi anakuambia hii ni nyumba ya kupanga, akasahau kwamba yeye ndiye anaishi humo. Msemo huo unasema Tengeneza furaha yako, Furaha haikutafuti kabisa!
ikitokea kuna jambo linakusumbua litakusumbua kwa muda kidogo sana kwani asilimia 90 umejizungushia ukuta wa furaha. Furaha yako unatakiwa kuitengeneza haiji bure. Hotoletewa kwa chupa kama uji unywe! Jipange.
ISHI.
