SHEREHE ZA SIKU YA WANAWAKE DODOMA KUPABWA NA MHE WAZIRI MKUU.

Mwenyezi Mungu ni Mwaminifu sana

HONGERENI KINA MAMA WA TANZANIA

HONGERENI KINA MAMA WA DODOMA

Naendelea kupitia matangazo mbali ya Sherehe kubwa za Siku ya Mwanamke Duniani hapa Tanzania ambazo mwaka huu zimekuwa na msisimko mkubwa sana na ambayo kwayo, utaweza kuona namna wanawake walivyojipanga nchi nzima. Hiki ni Kishindo cha MAMA SAMIA!

Kwa Mkoa wa Dodoma tumeona namna ambavyo Mgeni wa heshima katika kusherehesha siku hiyo atakuwa ni Mhe Waziri Mkuu Ndugu Majaliwa Kassim Majaliwa. Mhe Kiongozi wetu huyu atapata nafasi kubwa sana ya kujionea maendeleo wanawake wa Mkoa wa Dodoma wamefanya ikiwa ni pamoja na ufunguzi wa SACCOs ya Mkoa na shughuli nyingine nyingi za kijamii na kiuchumi. M

Mwenyekiti wa Jukwaa Mkoa wa Dodoma ndugu yangu Mary B Mabhaya ambaye amefanya kazi kubwa kwa kushirikiana na Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Madam Rose Sinyamule, katika kusimamisha majukwaa mkoani DODOMA. Nikiri kwamba, kulingana na taarifa ninazo patiwa kila mara na Mwenyekiti wa Jukwaa DODOMA ni kwamba DODOMA KUCHELEE sana.

Mungu awabairiki katika sherehe za siku ya wanawake kesho huko Dodoma.

Hongera sana Mkuu wa Mkoa Dodoma

Hongera sana Mwenyekiti wa Jukwaa Dodoma

Mama Samia Hoyeeee!

TUKO PAMOJA.

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *