UMMY MWALIM KUZIPAMBA SHEREHE ZA SIKU YA MWANAMKE MKOANI TANGA

Mwenyezi Mungu ni Mwaminifu sana

Wanasema na imeandikwa “Pepo Zetu zipo katika Miguu ya Mama Zetu”

HONGERENI KINA MAMA WA TANZANIA

HONGERENI KINA MAMA WA TANGA KWA MAANDALIZI MAKUBWA YA SHEREHE ZA SIKU YA MWANAMKE MKOANI HUMO!

Naendelea kupokea taarifa mbalimbali kutoka kwa wenyeviti wa Mikoa wa Majukwaa ya Uwezeshaji Wanawake Kiuchumi na maandalizi ya sherehe za Mwanamke yanavyoendelea nchi nzima. Nitoe taarifa kwamba huko mkoani wa Tanga, kulingana na taarifa niliyoipata kutoka kwa Mwenyekiti wa Jukwaa la Mkoa wa Tanga dada yangu na wajina wangu Fatma Hatibu, Menyekiti Bingwa kabisa amesema zipo sherehe mbili ambazo zitafanyika Tanga.

Sherehe za Kimkoa zitaongozwa na Mhe Joketi Mwegelo ambaya atashiriki katika sherehe hizo huko Wilaya ya Pangani, wakati huo huo usiku wa mwanamke utapambwa na Mhe Ummy Mwalimu Waziri wa Afya na  Mbuge wa Tanga Mjini.

Mwenyekiti wa Majukwaa Mkoa wa Tanga vilevile amenitaarifu kwamba, maandalizi ya sherehe Tanga niya khali ya juu huku wakiwa na mipango mbalimbali ambayo kwayo, itakwenda kuhakiksiha SACCOs Tanga inafunguliwa kwa kushirikiana na wadau wa Maendeleo.

Amesema pia wamejitahidi kushiriki katika utoaji wa huduma mbalimbali za kijamii katika Hospitali na elimu za ujasiriamali. Wana mashirikiano makubwa na  uongozi wa Mkoa kutoka kwa Mkuu wa Mkoa na viongozi wote na Afisa maendeleo ya jamii ambaye anawapa nguvu kubwa. Wilaya zote zitaadhimisha sherehe hizo kwa shangwe kubwa zikiwemo Wilaya ya Tanga Mjini, Pangani, Mheza, Lushoto,Korogwe, Handeni  na Mkinga.

Mdau wa maendeleo ambaye pia ni mjumbe Kamati ya utekelezaji Mkoa wa Tanga na Mbaraza wa UWT-Mkoa Bi. Jane Gonzalves nilivyomuuliza maoni yake  juu ya sherehe za siku ya Wanawake Mkoani Tanga alisema “TANGA HATUNAGA JAMBO DOGO- HATUPOI HATUBOI alisisitiza. Wao wanasherekea kutokea Pangani na Mgeni ni Mhe Joketi Mwegelo Katibu Mkuu UWT. Vilevile akisisitiza kwamba mashirikiano kati ya mwanamke na mwanamke mkoani Tanga yanazidi kuimarika.

HONGERENI TANGA

HONGERENI TANZANIA

HICHO NI KISHINDO CHA MHE RAISI Dkt mama Samia Suluhu Hassan

TANGA Hoyeee.

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *