Mwenyezi Mungu ni Mkarimu sana!!!
Sisi Binadamu ni lazima kila uchao tumshukuru kwa kila jambo. Sijakutana na wasomaji wa makala zangu muda mrefu saana. Mwaka Mzima wa Mwaka jana nilikuwa naendelea na majukumu mengine kwani mambo mengi mazuri yalinitokea, pia kama tujuavyo binadamu changamoto ni sehemu ya maisha yetu, na ni UTU pia, bila changamto hauwezi kukua, hivyo nilijipa utulivu wa kukaa na kushukuru Mwenyezi Mungu zaidi. Naomba Mwenyezi Mungu azidi kunipa kibali cha kuendelea kuwahudumia wanawake nchini na Duniani kote katika hali ya kuwajenga Ki fikra, Kubadilishana mawazo na kuelimishana. ELIMU HAINA MWISHO mimi nijifunze kweno=kwao na wao wajifunze kwangu.
Leo kwa ufupi kabisa nikianza makala zangu mbalimbali kwa wanaweke, nitaanza na suala la MAJUKWAA. Yanaitwa Majukwaaa ya Uwezeshaji Wanawake Kiuchumi. Umeshayasikia? Lazima uyasikie kwani ndio AGENDA kubwa ya mwanamke wa Tanzania leo. Kila mtu anapaswa kujifunza na kuyaelewa. Nitaandika kwa kirefu nafasi ya Uanzishwaji wake, Nani kayaanzisha na Kwanini yameanzishwa nikitoa mtazamo wangu kama ambavyo leo nimehojiwa na Radio One juu ya nafasi ya Majukwaa hapa nchini. Naamini nilizungumzia vizuri historia ya kutukuka ya wazo hili lilivyotokana na Mhe Raisi Dr Mama Samia Suluhu Hassani ambaye toka mwaka 2016 alianzisha majukwaa haya. Naitafuta Link ya mahojiano yangu ya Radio One leo na kuiweka humu ili muweze kujifunza maoni yangu kwa kwa kweli kumshukuru Mhe Rais kwa zawadi ya majukwaa. Makala zangu zijazo nitaeleza vizuri juu ya nafasi ya majukwaa katika kumuendeleza mwanamke kiuchumi.
Sherehe za mwaka huu nchi nzima, zimeamsha nafasi ya MAJUKWAA katika kumhudumia mwanake, Kila mwanamke alihitaji kutoka na kwenda kujifunza juu ya jitihada mbalimbali ambazo serikali yetu inafanya katika kumjenga mwanamke wa leo. YAPO MENGI YA KUJIVUNIA na sherehe za Majukwaa zimeandaliwa kila mkoa hapa nchini. Shime totoke kwenda kujifunza na kujijenga Zaidi.
Nimetoa ratiba ya Majukwaa Mkoa kwa Mkoa na nitashare taarifa za ratiba hizo katika Makala inayofuata.
