MWANA DADA EUTROPIA JAMES AFANYA MAPINDUZI KWENYE MAFUTA YA NYWELE NCHINI TANZANIA
Wanawake wa Tanzania ni Moto !!!! wanasema moto fire!
Moto wa kuotea mbali kwa Mipango, Akili na Mikakati
Ukimkuta mwanamke wa Kitanzania amejitambua UTAMPENDA kweli na vile hii lugha yetu ya Kiswahili ambayo imefanya watu wawe na uwezo mkubwa wa mawasiliano imefungua akili za watu wengi. UBUNIFU hujengwa na LUGHA! Asante KISWAHILI.
Hii nchi yetu ipo tofauti kabisa! Ina ubunifu wa khali ya juu! Ina watu na wananchi wanaojituma! Ni linchi likubwa sana. Lililosheheni neema za vitu vingi. Hasa watu! Wenye uweze upendo na akili kubwa. Mmoja kati ya maeneo niliyoyafanyia kazi kwa muda mrefu ni sekta ndogo ya SMEs. Nimekutana na rasilimali dhahabu, Rasilimali Fedha yaani watu ambao ni rasilimali. Migodi kabisaa. Katika SMEs kuna vipaji vya ubunifu bidhaa! wanasema Products Development. Watu huko kwenye ujasiriamali hawalali. Yaani huko ni kusoma, kujituma, kutengeneza na kuzalisha.
Mara hii nakuletea taarifa za mwana dada Eutropia James ambaye ni wale wa dada wanaotambulika kama wana “Beauty and Brain”. Kielelezo cha mwanamke wa kitanzania, mdada mrembo kabisa mdogo wangu huyu, akiwa na bidhaa zake za mafuta na vipodozi vya ngozi na mafuta ya nywele.
Katika Mkutano wa Kifungua Kichwa cha GS1 Tanzania, 2nd GS1 Tanzania Breakfast Meeting , madam Eutropha James alipewa bahati na Bodi ile kuweza kutambulisha bidhaa zake. Naye Mkuu wa UN hapa nchini pamoja na DG TANTRADE waliweza kushiriki kuzindua bidhaa zake.
Kampuni yake inajulikana kama
GRAZIE HAIR PRODUCT
ALIANZISHA MWAKA 2021
BIDHAA ZAKE NI<
Hair shampoo, Hair leave in conditioner, hair oil 100% organic
Nashauri uwasiliana naye kwa njia ya mtandao. www.grazielimited.com
HONGERA malkia wa nguvu
WANAWAKE WA TANZANAI HOYEEEEE.
Mwandishi wa Makala za wanawake ni Bi Fatma Kange, Ukihitaji kuandikiwa makala za kibishara unaweza kuwasiliana naye kwa no 0767 520 116
