MAMA MIA SOKO – WAUNGANISHANA NGUVU NA GS1 TANZANIA KUPELEKA BIDHAA ZA WAZALISHAJI AFRIKA NA DUNIANI KIMTANDAO.
Mama Mia soko ni SOKO Mtandaoni.
Utauza bidhaa yoyote kidigitali.
Mpango huu utamsaidia mfanyabiashara mzalishaji hasa mwanamke! Wanawake wote wazalishaji mpango huu ni wenu
Tanzania yetu ni nchi inayokuwa kwa kasi sana katika mendeleo ya uchumi wake na watu wake. Nchi hii toka Uhuru imepiga hatua mbalimbali za maendeleo. Mipango ya miaka mitano mitano na vichocheo vya sera pamoja na sheria mbalimbali zimeweza kuiweka Tanzania kwenye ramani kubwa sana hapa nchini.
Katika kuhakikisha, kwamba wananchi wa Tanzania wanapata nguvu ya mageuzi ya maendeleo ya uchumi wa Soko, Mhe Raisi Dkt Mama Samia Suluhu Hassan amekuwa, toka kuingia madarakani kuhakikisha kwamba sekta binafsi inafunguka ili iweze kuchochea makuzi ya uchumi wetu. Hiyo imetupa nguvu hadi sasa Mhe Waziri wa Viwanda ndiye mwenyekiti wa wenyeviti wa mawazi wa Biashara wa soko la Africa. TANZANIA TUNA FAIDA KUBWA sasa tunatokaje hapo?
Raisi amekwenda mbali zaidi kuhakikisha kwamba soko la Africa linasimama na wananchi wanaweza kuongeza kukuza masoko ya bidhaa zao. Ndio uchumi wa digitali unavyopigiwa dondoo kufahamika na nafasi yake kuchukuliwa na wazalishaji ili waweze kuongeza biashara zao.
Dorice Malle majasiriamali wa soko mtandao amekua na bidhaa kubwa ya Mama Mia Soko ambayo imeunganisha nguvu na GS1 Tanzania. Katika kuhakikisha kila bidhaa itakayouzwa kwenye soko mtandao hilo, ina Barcodes za GS1 Tanzania yaani GTIN zinazotambuliwa Duniani.
Ili kumlinda mlaji, wazalishaji wanahitaji kuhakikisha bidhaa zao, ndizo zinazouzwa kupita soko mtandao. Soko mtandao litadhibitiwa kuuza bidhaa ambazo sio feki kama zinakua zimevalishwa barcodes zenye mfumo. Sio Barcodes ni Barcodes itakayoweza kulinda bidhaa zako. Barcodes za GS1 Tanzania ni viwango vingine vya kimasoko vyenye mfumo unaoratibiwa kimataifa. Hakikisha bidhaa yako ina mfumo wa GS1 Barcodes
Linda bidhaa zako kwa kutumia barcodes za GS1 Tanzania ambazo pia zimeongeza mfumo a QR CODE. GS1 Soko ni mpango kambambe wa kuwaunganisha wadau wote na mama mia soko. Bidhaa zatu zitauzwa kwenye mtandao wa GS1 Tanzani ambao ni GS1 SOKO.
Tembelea ofisi za GS1 Tanzania kupata mpango huo au Ofisi za Mama Mia
Piga simu no 0767 520 116
Mpango wa GS1 SOKO na Mama Mia SOKO utakwenda kujenga wanawake nchini TANZANIA
Huu ni wakati wenu. Changamkieni FURSA.
Fatma Kange pamoja na mambo mengine ni mwandishi na huandika makala za wanawake na maendeleo yao kama sehemu ya kurudisha kwa jamii. Ukihitaji kuandikiwa makala wasiliana naye..
