SHEKHA NA BARCODES

MFUMO WA HUDUMA YA BARCODES KWA WANAWAKE WENYE VIWANDA -NCHINI

Katika mfululizo wa makala zangu na wanawake wa Tanzania juu ya biashara, uchumi na ustawi wao, leo katika andiko hili dogo nawaletea mfumo wa Barcodes na wapi pakuanzia ukitaka kupata huduma za Barcodes nchini? Wanawake mbalimbali ambao wamepata taarifa sahIhi juu ya mfumo wa barcodes wameutumia na kukuza biashara zao mfano wa wanawake hao ni kama akina Mama Alska-Jenipha Bashe, Shear Illusion -Shekha Nasser na Zoazoa Dr. Elizabeth Kalili. Kupitia ofisi ya GS1 Tanzania nimeweza kuwahudumia akina mama wengi sana hapa nchini, na mafanikio yao nimeyashuhudia. INAWEZEKANA. Barcodes ni huduma muhimu sana kwako wewe mwanamke mzalishaji.

Nimebahatika kufanya kazi kwa kipindi cha miaka 10 katika Taasisi ya GS1 Tanzania kama Mkurugenzi Mtendaji, niliahidi nikifika umri fulani nitasimama na kuanza kuwatengeneza wanawake wengine popote nchini na Duniani kwa ajili ya mambo ya msingi kwa ajili ya ustawi wao, kulingana na yale ntakayokuwa nimekutana nayo yenye nafasi ya kuwatengeneza wengine. Kila ninalolijua lenye manufaa kwa wanawake nitaliandikia na kulitangaza. Ninapoishi malengo yangu nimetengeneza mfumo huu wa mawasiliano kwa ajili ya kutimiza malengo hayo. Na hili lichukulieni kama Sadaka ndugu wasomaji wangu na wanawake wenzangu. Sadaka ya Taarifa- na wanasema “Information is Power”

Ikiwa wewe ni Mwanamke, Mjasiriamali nipende kukutaarifu kwamba, katika toleo la leo ukiwa ndani ya nchi yetu, kuna mambo mengi yanayoendelea, ipo mifumo mingi ya uwezeshaji lakini ili kutimiza malengo yako ya bidhaa zinazozalishwa, kuweza kuwa na sura ya kimataifa na kupata masoko ni muhimu kuzifahamu njia mbazo unatakiwa kuzijua ili uweze kupeleka biashara yako huko katika masoko ya ndani na nje. Bado nasisitiza Royal Tour itahitaji wanawake waliojipanga! Pateni taarifa muhimu na muweze kujipanga kimkakati. Tuweni wa kimataifa na Barcodes.

Nitatumia Picha ya Madam Shekha Nasser niliyompatika wakati fulani, miaka 7 iliyopita juu ya mfumo wa Biashara na Barcodes nchini, ambayo pamoja na mambo mengine Barcodes ilimtambulisha vyema sokoni na kuweza kusonga mbele. Barcodes ni nembo muhimu sana. Ukitaka kuielewa nembo hii ujue inavyo onekana, Barcodes ina alama kama ya mistari mistari katika bidhaa, Chukua bidhaa yoyote na itazame ukiona kuna nambari za mistrari basi hiyo ni barcdoes. Huduma hii unatakiwa uwe nayo ili uweze kuuza bidhaa zako nje na ndani ya nchi. Huu ni mfumo wa kidigitali wa masoko utakuweza kukusaidia kuuza katika supermarket nk. Kanuni au hatua za kuchukua ili kuwa na barcode ndizo hasa zinapelekea kuandika makala hii.

Bidhaa yako, unayotaka kuipa barcodes, itafiti kwanza, jua kanuni zote za kisheria ambazo zinakutaka kuzitimiza ili uweze kuingiza bidhaa yako sokoni. Bidhaa hutumiwa na binadamu ambao ni lazima wawe salama, ndipo suala la Viwango huingia kati. Sasa Taasisi kama TBS, Mkemia Mkuu, TRIDO zinaweza kukusaidia kukushauri katika kukupa mahitaji ya kimakakati katika kuizalisha na kuisimamia biashara yako. Kila mwanamke ambaye anahitaji kuuza bidhaa zake, ni muhimu kutembelea taasis hizo kwa ushauri.

Usajili wako, wa jina au kampuni kausajili BRELA. Brela ni taasisi muhimu sana, hutakiwi kuanzisha jambo nchini hapa kama halina usajili, NGO zina maeneo maalumu ya kusajili hivyo hivyo kwa kampuni na biashara. Wewe kama unataka kuanzisha biashara yoyote nchini, hatua ya kwanza Tembelea BRELA. Wana hadi Website. Watakupatia maelekezo yote kwa kina sana.

SIDO hakuna taasisi muhimu kwa kuchakata wazalishaji nchini kama hii, kama unataka kuwa mchakataji wa jambo lolote na kwenda kuanzia taasisi yako basi SIDO iwe kimbilio lako. Wanatoa mafunzo mengi mno, kuanzia Elimu ya kusindika Sabuni, Mafuta, Ushonaji, Usindikaji wa kila aina nk. Uzuri wa taasisi hii iko kila mahali nchini Tanzania yaani kwa maana ipo mikoa yote nchini.

Taasisi ya TRA- Kama umeshamalizana na BRELA, TBS, SIDO Nenda TRA kajichukule TIN yako bure kabisa. Kwani kwa sisi watoaji Barcodes mfumo ya Barcodes tunahitaj mzalishaji awe na TIN, LESENI YA BIASHARA NA CHETI CHA BRELA. Kwa mpangalio huu, ukiwa umeshamalizana na taasisi hizo wewe tembelea GS1 Tanzania-Ofisi ipo TIRDO Msasani Dar Es Salaam au tembelea kupitia: www.gs1tz.org, ili ujipatie Barcodes zako bila wasiwasi wowote.

Wanawake wa Tanzania ni muhimu kuchukua fursa za kibiashara kwani, taasisi zote zipo tayari kwa ajili ya kuwa hudumia. Mfumo wa Barcodes upo kazini na wanawakaribisha.

Wanawake wa Tanzania sasa kuchelee

Wanawake wa Afrika Walihitaji zaidi Ushirika.

2 thoughts on “MFUMO WA HUDUMA YA BARCODES KWA WANAWAKE WENYE VIWANDA -NCHINI”

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *