MTANZANIA- BI. DIANA MAGESA ASHIRIKI MAONESHO YA WOMEN INTERNATIONAL SHOW- CANADA

MTANZANIA DIANA MAGESA awatoa wanawake kimasomaso kwa kushiriki maenesho maarufu -“International Women Show” yaliyofanyika nchini Canada kuanzaia tarehe 3 hadi 11 May 2022. Maonesho hayo yanayofanyika kila mwaka, mwaka huu yalitimiza miaka 21 toka kufanyika katika jiji la Toronto Canada. Kwa Mtanzania Diana Magesa kushiriki katika maonesho hayo anafungua rasmi pazia kwa wazalishaji wengi kujipanga kwa ajili ya kushiriki mwakani na miaka mingine inayokuja. Wanawake wenzangu na wasomaji wa makala zangu za kila siku, Ofsi yangu tena leo imepokea mgeni huyu akiwa amekuja na picha zake lukuki na mavideo mbalimbali akionesha tukio hilo adhimu nala kupendeza huku jijini Toronto kama lilivyojiri. Mgeni wangu huyu mjasirimali wa fashio za bidhaa zinazotokana na taka mbadala la mabaki ya nguo na vifaa mbalimbali ni mbuni aliyejizoelea sifa kimataifa. Jukumu langu linabaki mmoja tu, ni namna gani tunaweza kuwapa taarifa watanzania wanawake wachacharikaji kama yeye kufaida kimataifa kama yeye na tuweze KUKUA. Diana ananiambia kwa kuringa kabisa na akijiamini Dada Fatma namnukuuu ” Kila bidhaa niliyokwenda nayo Canada imeuzika” Diana Magesa. Nilibaki heee mbona Hatariii! Ila nikamwambia usicheze na Royal Tour hiyo imetokana na image ya nchi yetu sasa ! TUNAUZIKA! Tunauza jamani. TUZIDI KUJIPANGA.

Kama mnavyofahamu, ukurasa wangu wa TWEA umejitolea kabisa kupeleka taarifa mbalimbali na fursa za akina mama juu ya taarifa za uchumi na masoko kwa wanawake wote nchini kwa lugha nyepesi sana. Kila utakachosoma katika ukurasa huu ni Mwanamke na Maendeleo yake. Wengine tujifunze kutoka kwa wanawake waliofaulu, au tujifundishe kufaulu kimaisha. Mipango ya kitaasisi yenye kumlenga mwanamke pia tutaitangaza kupita ukurasa huu. Kama unafursa yoyote ya mwanamke basi tutaarifu tutaitangaza.

Nchi yetu Tanzania ni nchi inayokuwa kwa kasi na inapaswa watanzani wengi wachungulie Fursa kimkakati. Katika kukua huko kwa nchi yetu kunahitaji wanawake wanaojitambua na kuchukua sehemu ya fursa mbalimbali zinazojiokeza ili waweze kujikomboa kiuchumi na kijamii. kukuwa kwa nchini hii kunahitaji mazingira wezeshi kwa wanawake kuunganishwa na MASOKO mbalimbali. Masoko hupatikana kwa njia ya Maonesho, Mikutano na Ubia wa kimkakati. Katika maonesho hayo ya International Women Show Canda Dada yetu Diana Magesa aliweza kuiwakilisha nchi yetu kwa kishindo! Akiwa na bidhaa nzuri sana, ambazo zimetokana na malighafi za kitanzania . Amekiri kwamba, alishanga kuona watu wengi wanajua Kiswahili pia kwa maana kiswahili ni lugha inayokuwa. Kila aliyepita akiona TANZANIA alimsalimia kwa salam ya MAMBO? kutoka kwa wanzungu au watu weusi waliotembelea maonesho jambo ambalo lilimpa faraja sana. TUJIPONGEZE.

Kilichomshangaza sana ni aina ya bidhaa na vitu mbalimbli vilivyooneshwa katika maonesho hayo, Maonesho hayo ni makubwa sana sana. Hata hivyo kwa sababu ya wimbi la Korona ni nchi chache za Afrika zilishiriki na wengi wa waafrika walioshiriki ni wale wenye uraia au vibali vya kuishi Canada. Kwa kuwa hapakuwa na muwakilishi kutoka Kenya wa Uganda anasema kwa kifupi yeye katika maonesho hayo ni kama zaidi ya kuiwakilisha Tanzania aliiwakilisha Jumuiya ya Africa Mashariki. Diana ANAJIVUNIA juhudi zake na lazima tumpongeze mwenzetu KAWEZA. Diana mwaya UMEWEZA BEST!. Mimi nimeweza kumpa hongera nyingi sana kwani yeye kaenda na jambo letu la ROYAL TOUR kwa vitendo. Diana Magesa kaitangaza nchi. Nat umpigie makofi.

Kwa upande wa bidhaa zilizotia fora katika maonesha hayo, ni bidhaa za miti shamba kutoka Indonesia hasa dawa za kutibu miguu. ambazo zilijizolea umaarufu sana kupitia maonesho hayo. Haya watu wa Tiba Aslia Jipangeni! Anasema Diana nchi ya Korea ilikuja na bidhaa zinazotokana na mabaki ya miti yaani zilizoongezwa thamani zilizotokana na magome ya miti na magogo yake pia, bidhaa hizo ni kama vile Bidhaa za Shanga, Picha za Ukutani, Mapambo mbalimbali nk. Amekiri baadhi ya bidhaa na vitu vingine ni vya kawaida ambavyo watanzania wanawea kushiriki bila shida yoyote. Yeye mwenyewe Diana Magesa amejikita kwa ubunifu wa bidhaa zinazotokana na nguo mfano Mashati, Skirt, Mabegi na ameniruhusu kutangaza thamani ya bidhaa na kiasi alichouza. Kikapu cha Mtwara alikiuza kati ya shilingi za kitanzania 81,000 kwa kikapu. Mwaka huu amekwenda na bidhaa za Vikapu vya Mtwara ambavyo ameviongezea thamani. Picha zake zinaonesha baadhi ya bidhaa ndogo ndogo alizokwenda nazo na zenye kupendeza sana.

Kinachotakiwa sasa kwa wanawake wa Tanzania ni kuanzia Sokoni, ili kutengeneza order za vitu mbalimbali ambavyo vinaweza kuuzika nchi mbalimbali duniani. Kupitia maoneshoa hayo Diana aliuza vitu vyake vyote alivyokwenda navyo ambavyo vikapu vya mtwra viliuzika vyote. alikwenda na Vikapu mia, Mashati ya Kiume mia, Vibano vya nywele, Malapa ya Batiki, Hereni, Mabegi ya safari, yamechangaywa na Jeans na Batiki. Mpunifu Diana kutoka Tanzania ni mtu mwenye uwezo mkubwa ambaye kwa undani unaona jinsi hamasa ya uchumi wa ushirika unavyotakiwa kuingia ndani yao ili aweze kufanya vizuri zaidi. Kupitia dhana ya Ushirika TANZANIA inaweza kuuza brand za DIANA dunia nzima. Amekubali kujifunza juu ya Darasa la Dhana juu ya Ushirika wa Viwanda wa Madirisha ili aweze kutumia mfumo wa ushirika katika biashara zake.

Ameomba kama kuna wanawake wanaotaka kushiriki katika maonesho mengine ya International Women Show- yanayofanyika Toronto tarehe 4 hadi 6 Novemba 2022. wajitokeze na kila mwanamke anayetaka kushiriki maonesho hayo anaweza kutuandikia twea kwa barua pepe ifuatayo info@twea.co.tz ili tumuunganishe na Diana Magesa kwa taratibu zinazohitajika.

Wanawake wa Tanzania sasa kuchelee!

Wanawake wa Afrika walihitaji Ushirika.

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *