Wanawake Mkoani Geita waanzisha Ushirika wa Ufungashaji Mchele
Tume ya Ushirika nchini imeamua kwa dhati kulivalua njuga suala la wanawake na viwanda kwa kuweza kufadhili mafunzo maalumu yaliyofanyika mkoani Geita kwa ajili ya kuwajengea uwezo wanawake wa mkoa wa Geita.
Kama mtaalamu wa ushirika huu mpya wa viwanda vya wanawake tuliweza kuhamasisha na kufundisha zaidi ya wanawake 200 waliohudhuria semina ya Mhe Mkuu wa Mkoa wa Geita Ms Rosermary Sitaki na kufanikiwa kupitia semina hiyo kuwaunganisha wanawake na hatimaye kukubaliana jina la ushirika huo ambao utakujulikana kama Madirisha Geita Rice Cooperative Society.
Wanawake hao walichangisha jumla ya shilingi 350,000 kwa ajili ya kufungua account ya umoja huo.
Uchumi wa ushirika wa viwanda vya wanawake unawezekana
Wasiliana nasi kupitia
AU tembelea ofisi za MADIRISHA zilizopo Tegeta Nyuki Dar Eas Salaam
Mwenyekiti ni Bi Rosemary Mgalula na Afisa Habari ni Annamary Kavishe.
