Wanawake wengi walihitaji elimu kubwa sana ya kuwatoa kwenye mashinikizo ambayo mengi yametokana na mfumo wa kimaisha uliopo. Mafunzo ya TWEA ya TWEA Personal Development Training hutolewa kwa vikundi au mtu mmoja mmoja katika kupata mwanga wa mambo ya msingi ambayo yanahita wanawake kutoka kwenye mazoea ya kimaisha ili waweze kuziona fursa na kuzitambua na kuchukua nafasi katika maisha ya kila siku.
Uwekezaji ni elimu pana ambayo inahitaji wanawake kuandaliwa kwanza kujua miundo mbinu mbalimbali ambayo itawafanya wawe! Yaani Watokee! Wawe ni wanawake wakubwa! “Mwanamke Imara Groups” ni kundi la akina mama ambalo niliitwa kama mtaalamu wa wanawake na maendeleo katika kuwakokota nilifanikiwa kuwapitisha katika mambo mengi sana, Darasa lilitawaliwa na vicheko na vilio! Vilio vya kujua miaka mingapi wamepoteza, vicheko vya maisha mapya wanaojiwekea. Nilifanikiwa kwa pamoja kuwafanya waazimie mambo kama yafuatayo:-
- Kundi lao litakaa kibiashara
- Watakuwa na ofisi
- Watakuwa na kiwanda cha ushirika na watatumia mfumo wa MADIRISHA
- Watashiriki maonesho ya 77
- Watashiriki ziara mbalimbali za kimasomo ndani na nje ya nchi.
- Wao kama binafsi wafanye mabadiliko kwenye maisha yao ya kila siku
- Wafanya mbinu gani za kutoa stress na KUISHI!
- WALIFURAHI SAANA
- Mimi nangoja matokeo.
Somo hilo nalitoa kwa vikundi na mtu mmoja mmoja. Namshauri mwanamke mmoja mmoja au kwenye kikundi kwamba waanze kujitambua kwanza ndio ukashiiriki katika uchumi wa Ushirika.
Mafunzo hayo yamefanyika tarehe 07.05.2022
Fatma Kange na mindset transformation kwa akina mama nchini Tanzania.
Wanawake Tanzania sasa kucheleee!
Follow me at @Kange_Fatuma

Mafunzo haya ni taa ya miguu ya Mwanamke ili aweze kuleta matokeo makubwa na kuacha alama katika maisha yake. Asante sana Fatma Kange Mungu aendelee kukutumia.
Grace karibu sana katika ulimwengu wangu wa wanawake! Naupenda ulimwengu huu nimeudadisi sana! Naona yale yote niliyoyagundua niyatoe kwenu! Ulimwengu wa wanawake una hadithi nyinge mno! una mengi mno! TUISHI TUKIJENGANA! Usiache kuhudhuria madarasa yangu na mwambie na mwengine. NAWAPENDA SANA.
Hongera dada yangu kwa kazi nzuri anakofanya kuhakikisha wanawake na sisi tunaweza na kuziishi ndoto zetu🥰🥰🥰🥰🥰🥰🥰🥰🥰🥰
Hongera dada yangu kwa kazi nzuri unayofanya kuhakikisha wanawake na sisi tunaweza na kuziishi ndoto zetu🥰🥰🥰🥰🥰🥰
Asante sana Jamila Rajabu kwa message yako. Mimi masuala ya wanawake nayachukulia kama hobby, nimeyatafiti kwa muda mrefu bila kujua nilikuwa nafanya jambo kubwa. Hii elimu yangu na uzoefu wangu nimeona niwape tu!Hebu tupeane mbinu, maarifa, ujasiri na heri. Mwisho wa siku maisha ya Dunia ni hadithi tu alijisemea Babu yetu na Riasi wetu kipende Mhe Ali Hassani Mwinyi. ISHI!
Pamoja sana
Barikiwa