Karibu sana kwenye mfululizo wa makala zangu ambazo zinajikita zaidi katika ulimwengu wa wanawake. Ulimwengu nilioamua kuufanyia kazi na kuiishi. Hatua mmoja na muhimu sana ambayo nimeona ni dadavue leo ni hili la “Wanawake na Mkwamo”. Wanawake sisi namna tulivyoumbwa ni watu tunaongozwa na hisia, hisia zetu zinatupeleka katika kuyaendea mambo yote yanayotuzunguka kwa hisia kali, kuanzia katika ngazi ya uchumi na masuala ya kijamii hususani kifamilia nk. Mtu yoyote anayesukumwa na hisia akipata MKWAMO huumia sana, na pengine anakuwa mwepesi kukata tamaa. Hiyvo ndio changamoto kubwa sana nimekutana nayo ambao kwa wanawake wangu ambao huwatengeneza katika program yangu ya “TWEA-Personal Development Training” na mara nyingi tunachambua mikamwo hiyo huku tukipeana njia mpya kabisha ya kuvuka vikwazo hivyo na kupita program hiyo tumetengeneza faraja kubwa sana kwa wanawake mbalimbali.
Hivi mwanamke ni nani? Jukumu za makala zangu ni katika hali kutoa mchago tu kwa ulimwengu huu pendwa, ulimwengu wa mwanamke katika kuwekana sawa. Kila mwanamke anayepitia changamto ya MKWAMO jua hauko peke yako. Ndio maana leo nawaletea makala ya namna ya kuvuka vizingiti, MKWAMO WAKO aidha ambao umetokana na kuchukulia vitu poa, au umewekewa na watu wanaokuzunguka au umetokana na wewe mwenywe kuchukulia mambo kiurahisi rahisi. Je Elimu uliyonayo inashidhwa kukupa unachotaka katika maisha yako? Unavizingiti lukuki. Sasa ili kuvuka vizingiti hivyo nataka nikupe chanzo cha VIZINGITI vinavyozunguka wanawake wengi, na kama kuna ambalo unaona sijaliweka sawa tafadhali niandikie kwenye comment hapo chini. Kuwa huru kuchangia mada zangu.
Katika maisha hasa kwa wanawake kuna wakati unapitia mikwamo mbalimbali, na unatafuta njia sahihi ya kujikwamua kutoka katika mikwamo inayokuzunguka. Mara nyingi mikwamo inaweza kukamwishwa na masomo yako uliyoyachukua yakishindwa kabisa kukusaidia kufikia malengo makuu ya maisha yako. Mikwamo mingine inaweza kuletewa na watu pengine wameshindwa kukuelewa kazi zako kwasababu mmekutana tu ukubwani, hamjuani na mkapelekeana kuzalisha chuki za hapa napale. Sasa leo katika makala hii ndogo ningependa kumsaidia mtu yoyote ambaye kafikia hatua hii ya kutoona njia sahihi ya kujikwamua na kukata tamaa kimaisha. Hebu tudadavue hoja zetu kama ifuatavyo.
Wanawake wengi wana mkwamo unao tokana na “Uchovu unaotokana na kazi uliyoifanya kwa muda mrefu”. Wanawake wengi kuna mahali akifika anakuwa amechoka na kazi ambayo kaifanya kwa muda mrefu, mara nyingi ukilifanya jambo mmoja kwa muda mrefu hukuletea hali ya kutokusikia faraja na kuhisi kama huna raha fulani hivi kwenye maisha yako. Hili ni kwasababu limekuchosha. Jambo hilo linageuka KIZINGITI kwenye furaha ya maisha yako. Huu ni mkwamo mkubwa inamaana kwakuwa wanawake tunaongozwa na hisia wanawake wengi ni watu ambao wanamaisha ya kulalamika bila kujua mazingira yanayomuuza ni ile khali ya kufanya jambo mmoja kwa muda mrefu. TAMBUA NA JITETEE!
Dawa yake ni kutafuta MENTOR! Na vile utamaduni wa MENTORSHIP nchini kwenu ni jambo kama geni, nakushauri nenda tafuta wanawake nguli wakupe siri za wao kufanya kazi kwa furaha na wanawezaje Kujiongeza kila uchao. Napenda sana kumfuatiila best yangu mmoja Dr Elizabeth Kalili na mambo yake. HIvi mama wa ZOAZOA Brand kweli kuna jambo linamchosha, mara ana kanisa, mara ana TV Progam mara ana Mafuta anauza. Kwa ujanja huu DR Elizabeth Kalili kavuka VIKWAZO. Namuona kama mtu ambaye kashinda MIKWAMO! Wapo akina mama wengi wa namna ya Dr Elizabeth na ni sisi linabaki jukumu letu tuwachukulie kama ma-MENTOR wakatutoe. Hebu ujifunze kutoka kwa wanaweke NGULI tunaoishi nao nchini Tanzania. Mimi nawatafute niwa promote kwa wasichana wanaochipukia. Kazi Ziendelee!!!!!!. Wewe mwanamke unayesoma hii makala UNA MENTOR kweli au ndio vile bora liende! Hebu Acha mambo yako.! JIONGEZE.
Vilevile kuna lile kundi lingine ambalo vizingiti vinatokana na kuomba kazi, mfano hili ni lile kundi la wasichana ambao umetafuta kazi kwa muda mrefu, hadi unajiona kama huna bahati. Umetuma CV wee lakini huna majibu . Khali hii huwapa stress kubwa sana graduates wasichana ambao wametumia muda wao mwingi kusoma, kwa matarajio ya kupata kazi za maofisini na unakutana na KIZINGITI kikubwa kama hiki cha kutokuitwa kwenye ajira, Khali hii huleta STRESS. Dawa yake ni mmoja to wewe mwana dada hebu -JIONGEZE! Kwa sababu, elimu uliyonayo iwe ni njia ya wewe kuingia kwenye sekta binafsi na kuanza kufanya biashara ambayo moyo wako unakutuma na FURSA zipo. Nawatangazia wasichana magraduate kwamba nchi ina fursa sana mpaka natamani niwatingishe mtoe hela! Yaani mnachotakiwa ni mindset zenu tu kujiongeza . TANZANIA ni nchi ya Asali na maziwa kazi imebaki kwenu, hii mikwamo ya kiajira ni MAMBO ya kufirika tu, hayana TIJA na hailingani na FURSA zilizopo nchini. Hebu jipangeni!
kizingiti kingine kinaweza kuwa kwamba, jambo ulilosomea Fursa zake ni chache, hakikisha unagundua mapema na ujifunze kujiongeza kwa ku somea ujuzi……. SKILLS tofauti tofauti! Jamani jamani hapa nchini kuna taasisi inaitwa VETA! VETA VETA! Veta kwa mfano hapa nchini Tanzania inakupa nafasi kubwa sana ya kusomea ujuzi mbalimbali wazungu wanaziita SKILLS. Nenda chuo chochote cha VETA kajionee kozi mbalimbali ambazo zitakupa mguu ya kutembelea katika maisha. Ukishapata miguu life become simple wenyewe wanasema. Pambana sana kuhakisha unapata ujuzi utakao kupa miguu na kukutoa kwenye MKWAMO uliaonao leo wa kukosa ajira na nenda kawe mtengeneza ajira.
La mwisho kabisa ni juu ya kuishi katika “Maisha hasi, Marafiki hasi”-watu hasi. Hii ni dhana ambayo maisha ya kiafrika hayakutupa nafasi ya kuyajua sana mapema kwa sababu tunaishi kwa UDUGU uliotukuaka. Uafrika unatufundisha kutakiana HERI! Kuombea Mema! Katika dhana ya UBUNTU kIla mtu hugeuka ndugu wa mwengine , kwa sasa maisha ya maendeleo yamezalisha changamoto mpya, maendeleo yanaleta SINTOFAHAMU na kutengeneza vijichuki vya hapa na pale ambapo ukiwa mwamamke lazIma ujue namna ya kuishi kwenye maisha shindani. Kila kinachokupitia kichukulie kama somo na TAFATUA miguu mingine ya kutembelea ikiwa ile unayotumia imekatwa. Kuwa na macho makubwa zaidi TAMBUA NA VUKA VIKWAZO vyako sasa! Kwa maelezo zaidi ya mafunzo ya USO KWA Macho na Nanma ya kujikwamua katika maisha tuandike info@twea.co.tz au tembelea www.twea.co.tz. Na ukawe mwenye furaha ISHI !
Mwanamke Nguli ni yule yanayevuka vikwazo. VUKA VIKWAZO VYAKO MAMA!. TEMBEA.
Tanzania sasa kuchelee.
Wanawake wa Africa walihitaji Ushirika,

Asante madam,. Nimeongeza mguu mwingine hapa baada ya kusoma hii makala.
Kikubwa nachokiona katika hii mikwamo, ni kukosa elimu ya “KUJITAMBUA”..
Mtu akijitambua…..ataelewa
-Yeye ni nani.
-Kwanini ni tofauti na mwenzake.
-Kwanini yupo hapa dunia.
-Nini afanye…(kiroho na kimwili) ili kutimiza kusudi la yeye kuwepo hapa duniani.
Madam Jane Isabela
Mpango mzima ni Kutembea. Nimependa sana ulivyoiweka hivyo
kUJITAMBUA ndio changamoto ya akina mama wengi. Falsafa Ongeza Mguu mwengine. Weka malengo VUKA!
Kila kilichoko chini ya jua, huota jua na vikwazo navyo vinaota jua.
Sasa kumbe hakuna lolote la kutisha. Nikuomba Mungu na kuvuka.
Bwana wee… TEMBEA. Jiongeze
Soma vitabu sahihi. Dawa yako, Heshimu Familia yako, Wapende ndugu zako, Kumbatia marafiki zako wa utotoni,
Watakupa nguvu, kama umeshikwa na changamoto yoyote anzia nyumbani. Farijika alafu toka.