Mgeni Rasmi

SIKU YA NYUKI DUNIANI NA MWANAMKE

“SIKU YA NYUKI DUNIANI”-Tarehe 21 Mei 2022 serikali imepanga kuendesha maadhimisho ya Siku ya Nyuki Duniani. Katika kilele hicho, kulingana na Tangazo lililotumwa Mgeni rasmi ni Mhe Mizengo Peter Pinda, Waziri Mkuu Mstaafu wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Mimi naweza kumuona kama Mzee wa NYUKI! Alituhamasisha sana kuelewa mdudu nyuki hapa nchini. Alitusisitiza kwamba-Nyuki ni Mali!!!. Jitihada zake kwa kweli zimezaa matunda.

Kama kawaida ya Blog yetu kuhusisha masuala mbalimbali yanayoendelea nchini na uchumi wa Mwanamke wa Tanzania kama sio wa Afrika kwa ujumla.

 Wanawake wenzangu mdudu nyuki ni alama ya ajabu duniani. Nyuki ni zaidi ya faraja kwa maisha ya uhai wa Dunia. Eti Kila tunachokula  kimechavushwa na nyuki!  Bila Nyuki inasemekana hakutakuwa na chakula Duniani. Ila nisiende huko zaidi, nije kwenye Nyuki na Uchumi wa Mwanamke.

Katika makala yangu iliyopita kuna sehemu ambayo niliandika kama wanawake wakimsoma nyuki na kuelewa umuhimu wake wa kuchukua hatua na kuishi maisha kama Malkia watapata faraja kubwa sana Duniani. Malkia nyuki ana faida kubwa sana ukimtafakari maisha yakemoja ya tatu basi Kuishi kwa faraja! Malkia wa Nyuki ni mtawala asiyenakifani. Pengine  kuiga japo kidogo wenzangu ha ha ha ha . Pia huko nako naona nisiende kwani kunahitaji tafakuri kubwa mno mara nyingine zinakwenda hata masuala ya kiroho. Ngoja niendelee na mada yangu…!

Nyuki huzalisha asali ambayo ni chanzo kikuu cha mapato kwa wanawake wengi waliopembezoni. Kilimo cha ufugaji wa nyuki ni rahisi kukifanya na ili wanawake tufaidike nacho ni muhimu kuelewa dhana ya Ushirika. Tukiwa na maushirika ya wafugaji nyuki naya wafungashaji wa Asali, tujue fika kwamba, siku hizi maalumu za kumzungumzia nyuki Duniani zitaturejeshea tabasamu kwa sababu tutakuwa na faida ya kwamba tumemuelewa Nyuki na tunafaidikaje naye. Sisi tufungashe asali ya Tanzania tuuze na tujikwamue kiuchumi. INAWEZEKANA.

Uoto wa Asili unaruhusu sana ulimaji wa kilimo cha Ufugaji wa Nyuki. Karibia kila maeneo nchini Tanzania yanaruhusu kilimo cha ufugaji nyuki. Ninashauri kwa kila mwanamke tushiriki sherehe hizo ili tuweze kujifunza namna bora ya kuendea fursa ya Nyuki. Mazao ya nyuki yanafaida ya kipato na kiafya duniani na kila mtu anayatafuta. Tuchukue Fursa. Nyuki hoyee!

Wanawake wa Afrika walihitaji USHIRIKA!

Tanzania sasa kuchelee

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *