Mwenyezi Mungu ni Mwaminifu sana
Kila jambo alifanyalo binadam ni Ibada.
Imeandikwa kwamba, Pepo zetu zipo chini ya nyayo za mama zetu”
Mpendwa msomaji wa Makala hizi za wanawake na maendeleo yao, ningepeda kukujulisha kwamba, katika kuundwa kwa majukwaa ambayo ni kazi kubwa aliyoifanya Mhe Rais Dkt Mama Samia Suluhu Hassan, muundo wake unazingita muongozo maalum ambao unasimamiwa na Wizara ya Maendeleoya Jamii Jinsia Wanawake na Makundi Maalum. Kwa upande wa Uongozi katibu wa Jukwaa letu Kitaifa anatokea Mkoa wa Shinyanga, Dr Regina Malima.
Asubuhi hii, na hasa nikiwa njiani kuelekea Kigamboni nimeongea naye kwa simu kunipa habari za Mkoa wa Shinyanga na Shangwe zao leo. SHINYANGA WAMEJIPANGA.
Akinitaarifu “Mwenyekiti sisi Mkoa wa Shinyaga leo Mgeni rasmi ni Mhe Christina Mndeme, Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga. Vilevile wanawake wa Mkoa mzima wa Shinyanga tunakutana Shinyanga. Wao wameundwa wilaya za Ushetu, Msalala, Kahama Manispaa ya shinyanga Shinyanga DC na Kishapu.
Kwa upande wa shinyanga, jukwaa lilishazindua mpango kazi wa Mkoa na wamefanya mengi katika kumuenzi mwanamke. Shinyanga ni mkoa pia unaoongoza kwa miradi ya wanawake.
Wilaya ya Ushetu imefanya vizuri mno wana Mradi wa kufanya usafi wa wanawake. Na wanakiwanda cha Kukoboa Mpunga na kufanya ufungashaji. Kwa ujumla shinyanga wanawake wanajituma sana. Alisisitiza.
Mafaniko ni kwa ujumla ni kuwa na mpangao mkakati wa Mkoa ambao pia umeuzwa kwa Wadau na vilevile kwa upande wa uongozi katika ngazi za Halmashauri jukwaa lina uwakilishi wa viongozi katika kila ngazi.
Mipango mingine waliyonayo ni kuendelea kutoa elimu kwa masuala ya Ujasiriamali na wanawake kuongeza usajili wa vikundi. Mkoa wa Shinyanga umetoa ardhi ya uwekezaji takribani kila Halmashauri. Aliongeza kuwa leo katika sherehe za siku ya mwanamke Duniani Jukwaa la ushetu wanapewa Ruzuku katika kuendelezaji wa miradi yao. Wanawake mbalimbali nchini tunachakujifunza Shinyanga.
Binafsi nawapongeza sana shinyanga kwa hatua kubwa walizopiga.
Hicho ni Kishindo cha Mama,
HONGERENI SAANA.
