MKOA WA DAR ES SALAAM WAZINDUA JUKWAA UWEZESHAJI WANAWAKE KIUCHUMI KWA KISHINDO.

Mwenyezi Mungu ni Mwaminifu sana

Kila jambo alifanyalo binadam ni Ibada.

MKOA WA DAR ES SALAAM WAZINDUA JUKWAA UWEZESHAJI WANAWAKE KIUCHUMI KWA KISHINDO

Uzinduzi wa Jukwaa la Mkoa wa Dar Es Saalam ni kielelezo kwamba sasa sekta binafsi ya Wanawake inakwenda kujipanga upya. Jukwaa La Mkoa wa Dar Es Salaam ndo kiunganishi cha kazi zote zinazofanywa na  serikali ya Mkoa katika kujenga uchumi wa Wanawake.

Mkuu wa Mkoa wa Dar Es Salaam Ndugu Albert Chalamila anakuwa kinara namba mmoja katika kuhakikisha kwamba Jukwaa hilo linazinduliwa akishirikiana na Mwenyekiti wa Mkoa wa Jukwaa Bi Fatma Kange, Mratibu wa Jukwaa Bi Zubeda Masoud na viongozi wote kutoka wilaya tano za Mkoa wa Dar Es Salaam kama vile, Temeke, Ubungo, Kinondoni, Ilala na Kigamboni. Wenyevieti wote wa mkoa wa Dar Es Salaam na sektratriate ya jukwaa kila wilaya wamajipanga kufanya kazi kimkakati.

Uzinduzi wa Jukwaa la Uwezeshaji wanawake kiuchumi ulifanyika  wakati wa sherehe za Siku ya Wanawake Duniani zilizofanyika katika Wilaya ya Kigamboni,  wilaya ya DC Bingwa kabisa  Bi Halima Bulembo. Katika  Sherehe hizo Bi Halima Bulembo alipewa Tuzo ya kutambua kazi zake.

Naye Mwenyekiti wa Jukwaa la Uwezeshaji Wanawake Kiuchumi Mkoa wa Dar Es Salaam akitoa salam za mkoa, alitamka na kumtaarifu kwamba ataunda Kamati Tendaji ambayo itafungua ushirikishwaji wa wanawake wenye taaluma tofauti tofauti katika watakao chochea maendeleo ya wanawake katika Mkoa wa Dar Es Salaam. Mkoa wa DSM ni mkubwa na unahitaji ushirikishwaji wa khali ya juu katika kumjenga mwanamke wa Mkoa huo. Bi Fatma Kange ameahidi kuchukua uzoefu wake kutoka sekta binafsi na kushirikiana na wenzake wa serikalini katika kujenga maendeleo ya wanawake nchini.

Sherehe hizo za siku ya wanawake zilipabwa na maandamano makubwa  ambayo yalipokelewa katika viwanja vilivyopo katika Wilaya ya Kigamboni. Taasisi mbali za umma na sekta binafsi ziliweza kuonesha mshikamano wao.

Pongezi Mkuu wa Mkoa wa Dar Es Salaam

Pongezi  Wanawake

Majukwaa Hoye.

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *