WANAWAKE DUNIANI WALIHESHIMISHWA KUTOKEA TANZANIA! DKT GETRUDE MONGELA NI ZAO NA TUNU TOKA TANZANIA – DUNIANI! HONGERA SANA KWA TUZO YA HALL OF FAME YA CLOUDS MEDIA GROUP.

WANAWAKE DUNIANI WALIHESHIMISHWA KUTOKEA TANZANIA!

MAMA DKT GERTRUDE MONGELLA NI ZAO NA TUNU YETU DUNIANI

KATIKA NDOTO ILE AMEISHI KUMUONA RAISI WA KWANZA MWANAMKE.

NDOTO IMETIMIA!

Hongera Dkt Gertrude Mongella  kwa tuzo ya Hall Of Fame ya Clouds Media Group.

Ulistahili pongezi!!.

Makala na Fatma Kange,

Pengine habari za nchi hii kubwa barani afrika hazijaandikwa vizuri. Tanzania ni fumbo lenye nahau nyingi katika nyaja mbalimbali za maendeleo ya nchi kwa ujumla na hata nchi za jirani Mchango mkubwa tuliotoa katika ukombozi wa bara la afrika haumithilili. Hii ni nchi kubwa sana. TUNAJIVUNIA.

Mara ngapi utaona katika ziara mbalimbali watu kutoka nchi mbalimbali wakija kujifuza  mifumo yetu ya namna tunavyojiendesha ?. Tumekuwa na ubunifu na uwezo mkubwa wa kupanga na kuibua mipango ambayo inatamanisha na kupelekea watu kujifunza juu ya mbinu na mipango yetu ya kiutawala na ubunifu.

Utaona sio katika nyanja ya Elimu, katika Michezo, katika ulinzi na usalama na katika masuala ya kijamii na Sekta ya Michezo, Tanzania imekuwa ni Kinara. Nchi kubwa sana yenye amani na utulivu ambao  kwa undani kabisa  ni kama zao kwa sasa kwa sisi watu wa viwanda hii amani yetu ni kama bidhaa “Products” inayoweza kuuzwa TUKAIFUNGASHE! …..Tunasifika kwa Amani. Hii ndio sifa yetu. Hii pia ni bidhaa jamani.  Gazeti la leo 25.03.2024 la Uhuru ukurasa wa mbele linasoma “ Tanzania ya tajwa mfano mzuri masuala ya Amani”  linanipa nguvu ya kuyasema haya wakati naandika hii makala yangu. Bado nasisitiza Amani ya Tanzania ni bidhaa TUKAIFUNGASHE TUKAIUZE!

Pengine  amani yake ni chimbuko kutoka kwenye mifumo yetu ya kiutawala hasa dhana ya nyumba kumi kumi watu wakajifunze kwenye mfumo wetu. Naamini Amani yetu inaanzia hapo. Huu ni mtizamo wangu binfasi tu. Nchi ya Tanzania ni familia kabisa. Watu tunaishi kama wanafamilia. Tutaiita Familia ya watu wa Tanzania. Katika Gazeti la Uhuru  linamnukuu Raisi Mwinyi akisema “Tanzania ni nchi yenye watu wenye Imani tofauti za kidini lakini wanaishi pamoja kwa kuvumiliana, kushirikiana na kupendana.  Gazeti hili linasababisha kuyapa nguvu mawazo yangu na kuzidi kusadiki kwamba sisi ni familia mmoja inayotakana na uwepo huu wa amani. We are indeed a beautiful family!!

Upande wa maendeleo ya wanawake hakuna nchi itakayoweza kuzungumzia uwezesahi wa wanawake na kujenga nguvu ya wanawake kiuchumi pasipo kuitaja TANZANIA!!! Hapatatokea katika maendeleo ya wanawake duniani na mipango mbalimbali ya kumuinua mwanamke kiuchumi na kijamii hata kisiasa pasipo kuitaja Tanzania hasa uongozi uliotukuka wa Dkt Getrude Mongella ambaye ndiye kinara wa mkutano mkubwa sana  wa mapinduzi ya wanawake na uchumi , kupita Mkutano maarufu ya Beijing Conference miaka 25 iliyopita. Mkutano ulioleta msisimko mkubwa na wa kukumbukwa katika kumjenga mwanamke duniani. Kikubwa ukubwa wa nchi hii unakuja kwa binti aliyezaliwa Ukerewe, Dkt Getrude Mongella kuweza kuwa kinara wa mkutao huo.

 Tunaweza kumchukulia poa, kwakuwa pengine ni Ukerewe! Si tumepazoea! Si kikwetu kwetu! Ukerewe hapo tu! si ni mwenzetu huyu! Ila katika mazingira ya ajabu kabisa binti huyu wa ukerewe ndiye kinara wa wanawake na uwezeshaji wao kiuchumi na katika Nyanja mbalimbali  za maendeleo huko Duniani, Dkt Getrude Mongela  ametambulika sana  na kwa muda mrefu, hadi kuasisiwa kwa Tuzo inayotolewa kwa jina lake la Gertrude Mongella Award inayotolewa kila baada ya miaka miwili na BPW kwa kuenzi kazi kubwa aliyoifanya ya kuendesha mkutano wa Beijing Conference mwaka 1995. Mkutano huo ulikuwa wa nne wa Umoja wa Mataifa wa juu ya Wanawake.

Mama, Dkt  Getrude Mongela alizaliwa Tarehe 13 Mwezi Sept 1945, huko Ukerewe na ameishi kufanya kazi mbalimbali ndani na nje ya Tanzania. Ana hisitoria nzuri iliyompelekea hadi kwenda  kuwa Raisi wa kwanza wa Bunge la Bara la Afrika. Kwa ujumla itoshe kusema Dkt Getrude Mongela huwezi  ukamuandika ukamaliza. Ni  mtu mkubwa ambaye katika ulimwengu wa wanawake yapo mengi amefanya na anayoweza kuenziwa nayo. Tuzo nyingi kapata na katambuliwa sana katika maeneo tofauti tofauti huko duniani kote.

Tuzo ya Clouds Media Group, Tuzo bora kabisa  hapa Tanzania juzi  imeweza kuwa daraja lingine kubwa la kumheshimisha mwana mama huyu kinara na nguli wa maendeleo ya wanawake duniani.  Inanikutanisha na taarifa alizotoa mwaka jana Mhe Waziri Dkt Doroth Gwajima juu ya maendeleo ya wanawke katika tuzo hizo hizo za Malkia wa nguvu Mwaka jana. Namnukuu “Waziri Gwajima amesema hapa nchini wanawake wamekuwa na mchango mkubwa katika uchumi wetu ambapo kitaifa asilimia themanini (80%) ya nguvu kazi ya Sekta ya kilimo ni wanawake na wanawake hawa huzalisha asilimia sitini (60%) ya chakula chote hapa nchini”

“Katika baadhi ya familia, wanawake ndio wahimili wakuu kwa maana ya upatikanaji wa chakula, mavazi na huduma nyingine za kijamii zikiwemo za kuwapeleka watoto shule na za afya kwa maana ya kuwahudumia wanafamilia ambao ni wagonjwa”. Amesema Waziri Gwajima.

Maneno hayo ya Dkt Gwajima yanatafsiri  kwa upana nafasi ya Dkt Gertrude Mongella  katika kumpambania mwanamke kupitia malengo makubwa ya Mkutano wake aliousimamia huko Beijing China Na kupitia mkutano huo, kumekuwa na matokeo mapana zaidi katika jitihada za kumkomboa na kumuenzi mwanamke. Aidha   matokeo ya athari za mama huyu wala huwezi kupishana nazo kwani  unaziona kwa macho….. Nchini Tanzania tuna jambo letu! Tunalo jambo kubwa sana la kujivunia. Ni kwa mara ya kwanza nchi kuwa na Raisi wa Kwanza Mwanamke! Ambaye si mwengine ni Dkt Mama Samia Suluhu Hassan. Nuru na Kipenzi cha wote!  Kwa maana nyingine kaiishi ndoto ya  Dkt Getrude Mongela! Mungu ni mwema siku zote!! 

Kwa  maisha yoyote ya kibinadamu naamini  huwa ni furaha kubwa na kumshukuru Mwenyezi Mungu kwa muota ndoto yeyote  kuishi na kuona ndoto yake ikitimia. Mabadiliko na athari ya jitihada za kumjenga mwanamke wa leo   zimekuwa nyingi duniani kote. Ikumbukwe  hadi nchini kwake Tanzania Dkt Gertrude Mongella Mwenyezi Mungu ananguvu, kwani yeye anaishi kuiona ile tija hata ndani ya nchi yake mwenyewe kwa jitihada zile, kuleta Raisi wa kwanza mwanamke. MWENYEZI MUNGU NI MKARIMU SIKU ZOTE!

Naamini kabisa kwamba, Mama Mongela atakuwa ni mtu mwenye TABASAMU kubwa moyoni ….pale anapoitimiza ndoto hiyo huku ikisheherekewa kwa shangwe za wanawake wote wa Kitanzania wanavyo mfuatilia Mhe Raisi wa Kwanza Mwanamke Dkt Mama Samia Suluhu Hassan. Furaha yake kwa tuliohudhuria tuzo hizo za Clouds Media tuliiona! Namnukuuu “Kwa Tanzania kuwa na Raisi Mwanamke haya ndiiyo tuliyoyataka” Akiongea na tabasamu kubwa sana. Alisisitiza watu waendelee kumuunga mkono kwa vitendo kwani anastahili kuungwa mkono Raisi wetu Tunu ya wanawake wa Tanzania na Afrika.

Jukwaa la Uwezeshaji wanawake Kiuchumi ambalo ni jukwaa lililoanzishwa na Mhe Dkt Samia Suluhu Hassan kwa upande mwingine linatafsiri kwa mapana kabisa na  kwa upeo wangu kazi kubwa iliyoanzishwa na Dkt Gertrude Mongella kimataifa.  Dkt Mama Samia Suluhu  na dhana yake ya Kazi iendelee inabeba dhima nzima ya Beijing Conference yaani kazi yake ya kumujenga mwanamke duniani kote. Matokeo chanya ya Mkutano wa Beijing Conference ambaye mwenyekiti wake alikuwa  Dkt Gertrude Mongella inaendelezwa na Mhe Raisi wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupita Majukwaa ya Uwezeshaji Wanawake Kiuchumi na dhana yake ya 4rs kwa vitendo. TUPEWE NINI WANAWAKE WA TANZANIA?

Majukwaa haya ambayo yamewekewa mfumo unaoanzia kutoka ngazi ya Kijiji/ Mtaa kwenda ngazi ya Kata na hatimaye ngazi ya  Wilaya na Mkoa yana ulezi na mfumo wa kiserikali uliothibitika. Kila Mwanamke anawajibu wa kujiunga na majukwaa hayo yanayotokana na ndoto kubwa ya kumjenga mwanamke iliyoanzishwa na Mhe Raisi Mama yetu Kipenzi Dkt Samia Suluhu Hassan toka mwaka 2016. Wanaweke kupitia majukwaa haya watapata manufaa makubwa sana, ambayo tunazidi kuyatangaza. Mambo ni mazuri sana.

Kama mwenyekiti wa Majukawa nchini Tanzania na kwaniaba ya viongozi wote wa majukwa Taifa na ngazi zote za Mikoa hadi Wilaya, Kata na Mitaa, napenda kwa pekee kumpongeza Dkt Gertrude Mongella   kwa kupewa tuzo  na vile vile kwa Clouds Media Group kwa namna mlivyoweza kumfikiria Dkt  Mongela na kumpa Tazo aliyostahili tuzo ya heshima Hall Of Fame.  ULISTAHILI SANA. UNASTAHILI SANA. Mwenyezi Mungu azidi kukubariki na kukupa umri mrefu duniani. AMINA.

Fatma Kange pamoja na mambo mengine ni mwandishi wa makala za wanawake na mfuatiliaji wa masuala ya maendeleo ya wanaweke hapa nchini na duniani kote. Endelea kufuatilia makala zake katika ukurasa wake wa TWEA ambao huandika makala mbalimbali za wanawake.

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *