Mwenye Mungu ni Mkarimu
Hutenda kwa wakati wake .
KUTANA NA ENG. LILIAN MWANGOKA MSTAAFU WA TCRA ALIYEAMUA KUSIMAMIA WANAWAKE NA VIWANDA KUPITIA USHIRIKA WA VIWANDA VYA MADIRISHA.
Eng. Lilian Mwangoka ni mstaafu wa TCRA ambaye ametumikia eneo lake la kazi kwa muda mrefu kwa zaidi ya miaka 30 ambaye amelitumikia Tiafa kwa upendo uliotukuka akianza kazi zake baada ya kufuzu mafunzo yake kutoka Chuo Kikuu Cha Dar ES salaam enzi hizo. Lilian ndio kati ya wanawake wa chache wa kwanza kwanza wa nchi yetu waliobebea katika masomo ya science. Baada ya kumaliza chuo kikuu miaka hiyo aliajiriwa na eneo lake la kwanza kufanya kazi ni ndani ya Jeshi la Polisi. Yeye ni mtaalam wa kurusha mitambo na kusimamia mifumo ya mawasiliano kwa njia ya masafa. Alipo malizia ajira yake hiyo baade alijiunga na Kampuni ya simu Tanzania ambapo alifanya kazi kwa miaka 9. Mabadiliko na namna sekta ya mawasiliano ilivyozidi kukua ndipo baada ya kuanzishwa aliweza tena kuingia katika mamlaka ya mawasiliano kwa ambapo alifanya kazi kwa miaka kumi na sita 16
Eng Lilian Mwangoka baada ya kustaafu kwazi kwake mwaka 2022 alijiunga na Ushirika wa Viwanda vya Wanawake vya MADIRISHA uliojipanga. Ushirika huu umeamua kuisimamisha SACCOs yake ambayo imeanza kutoa mikopo kwa wanachama wake.
Katika ushirika huu, lengo ni kuusambaza ushirika huu kwa wanawake katika ngazi mbalimbali za kiuchumi ili uweze kuwasaidia kujiongezea kipato.
Katika harakati za kuhakikisha wanawake wengi wanajifunza na kujiongezea kipato chao, chama cha ushirika wa viwanda kwa mara ya kwanza kilianzishwa mwaka 2020 kwa lengo ya kuingiza viwanda vya wanawake kwenye ushirika yaani Tanzanai kuwa na Cooperative Enterprises.
Eng Lilian Mwangoka, atakuwa msaada mkubwa kwa ushirika huu kwani, analeta uzoefu wake wa utendaji wa serikalini katika kuwasaidi wanawake walioamua kujitafuta hapa nchini.
Amepokelewa na bodi ya Madirisha Women Cooperative Society kwa moyo mkunjufu tukisubiri ajenge na kuratibu masuala ya ushirika wa viwanda kimkakati.
Kwa wanaohitaji kupata mikopo na kuwa wanachama wa MADIRISHA SACCOs wasiliana na Mhamasishaji wa masuala ya ushirika huu Bi Annamary Kavishe
Hongera Eng Lilian Mwangoka
Karibu Madirisha.
