Mwenyekiti wa Jukwaa La Uwezeshaji Wanawake Kiuchumi, Bi. Fatma Kange,
Ashiriki Futari Maalum ya
Mayatima,
Wajane na
Watoto wenye mahitaji Maalum iliyoandaliwa na BAKWATA-JUWAKITA.
Mhe Mufti BAKWATA aliweza kufungua Ifatar hiyo kwa DUA.
KATIKA IFTAR hiyo baada ya Risala ya JUWAKITA,
Mwenyekiti ameahidi kuwasaidia Umoja wa Wanawake wa Kiislam Kutimiza Malengo yao.
Jambo la Msingi
- Kuhakikisha Umoja huo Unaratibu, Kuundaa MFUKO MAALUM wa maendeleo ya Wanawake wa Kiislam Nchini Tanzania
- Kuhakikisha wanawake wa Kiislam wanajikita kwenye uchumi wa Ushirika, ili kukusanya nguvu na kujitegemea
- Wanawake wa Kiislam wanastawi kwa kuweza kushiriki katika huduma za kibenki ili waweze kumudu gharama za maisha na kujiongezea kipato, kwa kufuata fursa zilizopo.
- Kuwasaidia JUWAKITA katika azma ya ya kutimiza ndoto ya kuwa na jengo kubwa la kibiashara
- Mwenyekiti pia alifurahia Adhma ya JUWAKITA ya kujenga Hospitali yao. Aliwaambia mfuko wa maendeleo, ya wanawake utaweza kuwa, mwarubaini za changamoto za wanawake wa kiislam katika kujifanyia maendeleo yao.
- Mwenyekiti pia aliwahakikishia JUWAKITA, katika Jukwaa la Uwezesheji Wanawake Kiuchumi analichukua JUWAKITA KAMA JUKWAA MAMA litakalo simamia maendeleo ya Wanawake wa kiislam nchini na ameahidi kufanya kazi na JUWAKITA
- ALITOA CHANGAMOTO YA NAMNA GANI WANAWAKE WA KIISLAM kukaa na kucelebrate Urais wa Mama Samia, na kuandaliwe Kongamano la kutafakari maisha Bora ya Mhe Raisi kwa Wanawake na mabinti wa Kiislam katika kuwapa nguvukitimiza malengo yao. JUWAKITA bado wanakazi ya kufanya kuandaa tafakuri ya kushangilia Maisha ya Mwanamke wa Kiislam, kwa kufikia ngazi ya Uraisi Nchini na Africa, na Duniani Kote.
- Katika Futari hiyo pia ilifanyika, DUA MAALUM ya kumuombea Mhe Rais, Dr Mama Samia Suluhu Hassan, na Serikali nzima na viongozi wote
- Kugawa Nguo za Iddi kwa Wajane, Mayatima na Watoto wenye Ulemavu.
Aidha Mwenyekiti wa Juwakita Bi Mariam Mtambo alisisitiza Nia yake kubwa ya kuwaona wanawake wote wa kiislam wakiwa NADHIFU kwani Uislam ni Usafi. “Al Islamic Nadhifuu”
Alisisitiza.
Kwaniaba ya Viongozi wa Mwajukwaa, Bi Fatma Kange alitangaza kila Jukwaa lenye kuhudumia wanawake nchini katika ngazi zizote kuendelea kujitambulisha kwa Waratibu na Viongozi wa Majukwaa Nchini ili taarifa zao ziweze kuunganishwa katika mipango na upimaji wa matokeo ya Serikali. Aliahidi kuandaa kongamano, la viongozi wa Majukwaa mbalimbali nchini, ili Kufahamiana, kujipima na kujiongeza ufanisi kwa wanawake katika kujiletea maendeleo yao wenyewe.
Wasalamu.
