KUTOKA KUFANYA KAZI NBC BANk HADI KUWA KATIBU WA TAWI WA UWT KATA – KATA YA BUNJU.
Mercy Mgole Mukama ni mwanamke wa Makamu ambaye namtumia leo kama kelelezo cha kujenga wasichana wanaojitafuta. Kila kazi unayoifanya iheshimu. Kwani uzoefu wako wa kwanza unaweza kukupa miguu mingine ya kupambana na maisha haya ya kilasiku.
Mercy Mukama ambaye tawi lake kwanza lilikuwa NBC Bank House DSM na hatimaye kuhamishwiwa NBC Bukoba Kashozi Road ndilo lilio mkutanisha na baba watoto wake mzee Gamba Maugira. Mungu alimjalia watoto watatu ambao nao wanafanya vizuri. Baada ya kuacha kazi za bank alijiingiza kwenye siasa na kuanza chini kabisa kwenye matawi ambapo alijifunza uhamasishaji. Kazi hiyo imememfikisha hadi leo ni kati ya viongozi kuntu wa wanawake wa Kata ya Bunju kama katibu Kata wa UWT kata ya Bunju. Katibu mwenye Upako! Kicheko.Akitaka lake linakuwa.
Nafasi hiyo ilimpa kazi ya Mjumbe wa Mkutano Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni kwa vipindi viwili kutokea Tawi ambao hadi kufikia sasa ambapo ni Katibu wa UWT Kata Bunju. Tumpe mauwa yake! Kata ya Bunju ni yenye wanawake wengi na mahiri. Unapoluwa katibu wa Kata wa UWT Bunju lazima tukuheshimu.
Kinachovutia katibu huyu ni ufanisi wa kazi ambo umepelekea kupata tuzo za Wilaya Mara mbili kama katibu Kata mwenye ushawishi na mwenye wanachama wengi.
Mercy pamoja na mambo mengine ni kati ya wale wanoitwa Charistimatic Leaders, watu wadini husema wana upako ha ha ha! Upako wa Mercy ndio unaonifanya nimtatute kujua mbinu za uongozi anazotumia na kupata mafanikio hadi tuzo ndani ya chama chake cha CCM.
‘Vijana wengi hawasomi, soma katiba zote mbili za chama na jumuia zake ili uweze kusimamia yale unayoenda kuongoza. Uongozi bila kusoma haufiki popote. Unapotaka kuwa mwanasiasa lazima ujiendeleze’ nanukuu. Alielezaa namna alivyosoma kujiendeleza na kuhakikisha anajua Kanuni na Katiba ya Chama, huku akinitolea katika pochi yake katiba zake ambazo zimechakaa zinaonesha kwamba, kweli mwenzetu huyu ni msomaji.
Sasa hivi ni mhamasishaji wa bidhaa za New Life ambazo zinamuingizia kipato katika maisha yake ya kila siku, Mercy ni kati ya wale makatibu wa UWT Bingwa kabisa, Tumpe maua yake.
Fatma Kange pamoja na mambo mengine ni mwandishi wa makala za wanawake amepanga kutumia wanawake wanachipukia kupata mentors wa kuwaongoza katika maisha yao.
