MPANGO MAALUM WA KUCHANGIA KIWANDA CHA UACHAKATAJIWA KARATASI ZILIZOTUMIKA. BELTA KAZIMOTO ANAKARAIBISHA WADAU
Vijana wengi wanatafuta ajira.
Vijana wengi wanajitafuta
Vijana wenye hadhi ya Belta ndio watakaushinda matikisiko wa AJIRA
AJIRA HUTENGENEZWA! KIJANA amka na kajitengenenzee ajira yako
Ishi ndoto zako!
Belta Kazimoto ni binti aliyeamua kuzitafatuta fursa kwenye mazingira na kujisomea ujuzi wa elimu juu ya uchakataji wa karatasi zilizotumika katika Uganda Industrial Research Institute . Belta ni msomi aliyesomea degree yake ya kwanza Makerere Univercity na kumaliza mwaka 2019 na kuanzisha kiwanda mwaka huo huo 2019. Belta amejizatiti katika biashara yake ya kuzalisha karatasi hadi kufikia uwezeo wa kutengeneza Daftari, Karatasi za kufungia vitu mbalimbali.
Ameweza kuajiri hadi vijana wenzie 5 ambao hufanya uzalishaji katika kiwanda chake kilichopo huko Mbagala Mzinga jijini Dar Es Salaam. Kiwanda hicho ambacho nacho amechangiwa baada ya kushiriki shindano la COSTECH mwaka 2019 ambayo ulikuwa mradi wa Dar Technohama Business Incubator DTBi na baadae baba yake mzazi akamjengea chumba cha uzalishaji. Baadhi ya vifaa vya awali alipatiwa na COSTECH. Biashara yake imeanza kukua.
Katika hali ya kuikuza biashara hiyo ambayo imeanza kumuingizia kipato, Belta alimtembelea Mwenyekiti wa Jukwaa la Uwezeshaji Wanawake Kiuchumi ambao kwayo, alihitaji kutembelewa na mwenyekiti kujifunza na kuona anaweza kumsaidiaje kuendeleza biashara yake. Mungu alijalia na Desemba mwaka jana mwanyekiti bi Fatma Kange aliweza kutembelea kiwanda hicho na kujionea kazi kubwa inayofanywa na binti huyo pamoja na wafanyakazi wake. Kilichomvutia mwenyekiti ni bidhaa ambazo zinazalishwa kiwandani hapo. Mifuko, Madaftari nk
Belta aliweza kutembelewa na kuonesha changamoto za mashine ambazo zinahitaji kuongezwa, Mixer Kubwa kununuliwa na vifaa vingine muhimu. Anahitaji jumla ya shilingi 50Mln katika katika kuhakikisha biashara yake hiyo inaongezeka
Nimeamua kuandika hili makala, kwani belta amenigusa katika maeneo muhimu sana, kwanza ni kijana ambaye ameamua kuhakikisha anapambana na ajira kwa kujitengenezea kipato. Vile vile anaajiri vijana wenzake. Lakini kubwa kabisa kama mwanamke anatukumbusha umuhimu wa kujenga majukwaa ya uwezeshaji wanawake kiuchumi kwa kutafuta na kuungana na wale wanawake ambao pia wameanza kuonesha mwanga katika jamii, Mwisho ni namna kuwa ukubwa kabisa anavyo muunga mkono Mhe Dkt Mama Samia Suluhu Hassani katika kujenga sekta binafsi, na lingine ni vile anavyofanyia kazi hii katika sekta ndogo ya mazingira. Mazingira imekuwa changamoto kubwa lakini pia ni fursa. Belta ameweza. Tunahitaji kumtia moyo.
Belta Kazimoto ameonesha uthubutu ambao unahitaji kuungwa mkono na katika harakati za kuhakiksiha kiwanda cha Belta Waste Paper Recyclers kinatoa mchango wake anahitaji ndugu jamaaa na marafiki tumchangie mwanadada huu aweze kutimiza ndoto zake.
Mwenyekiti wa Jukwaa la Taifa ameshamuunga kwenye mfumo wa Barcodes, kamuunganisha na TIRDO ili aweze kupatiwa ujuzi na Gazeti la Mwanachi nao wameonesha nia ya kumuunga mkono. TWENDENI PAMOJA
Belta anaweza kupatikana kwa simu no 0757 55 3102 ili aweze kutoa ufafanuzi kamili wa mradi wake huo. Wanawake TUNAWEZA
Tumuunge mkono Belta Kazimoto.
Kijana mchapa kazi!
Je unamawazo yoyote ya kumuunga mkono? SHIME TUTOKEJE HAPO.
Fatma Kange pamoja na mambo mengine ni mwandishi wa makala za wanawake na maendeleo yao.
