Mwenyezi Mungu ni Mkarimu
amtumainiye Mwenyezi Mungu Hafi Maskini
MJUE DIWANI ANNA LUKINDO WA KATA YA MBEZI JUU- JIJINI DAR ES SALAAM KUTOKA MUUZA DUKA HADI UDIWANI!
Diwani Anna ndio jina lake maarufu kutoka katika kata ya Mbezi Juu! Ukisikia Mhe Diwani Anna ujue ni Diwani wa Kata ya Mbezi Juu.
Mbezi juu ni kata ambayo ipo katika jimbo la Kawe. Jimbo la Kawe ni maarufu kwa historia yake ya Uwakilishi Bungeni. Katika Tanzania yetu, Kawe ndio homa ya nchi hii linapokuja swala la uchaguzi mkuu. Majimbo yote yatashinda lakini Kawe ni nani mwakilishi ndio hoja inayoumizaga vichwa! Kwa wafuatiliaji wa masuala ya siasa za Tanzania mtanisahihisha hapo.
Wakati wa Uchaguzi wowote Tanzania macho, masikio moyo sauti zote watu huelekeza jimbo la Kawe! Jimbo la kawe wanasema ndio jimbo la washua sina uhakikia. Ila ndani ya jimbo hilo kuna hadithi iliyojificha ya diwani pekee mwanamke Mhe. Diwani Anna Lukindo. Mwanadada mahiri kutoka mkoani Tanga anayefanya vizuri jijini Dar Es Salaam.
Ni jimbo ambalo kila wakati wa uchaguzi unapofika huwa linafuatiliwa sana. Ndani ya Jimbo hilo kuna hadithi tamu. Hadithi ya Diwani Mwanamke pekee wa kata Jimbo zima! Binti mdogo Diwani wa Kata ya Mbezi Juu, ali maarufu Diwani Anna.
Udiwani wa Kata ni udiwani wa kupambana nje uwanjani. Unatofuati kubwa sana kati ya ule wa Viti Maalum na huu wa Kata. Ukitaka kupata udiwani wa kata unapita kwanza kwenye kura za maoni alafu utakwenda kushindana na timu pinzani wakati wa uchaguzi. Diwani Anna Lukindo ni kati ya Diwani wakata walioleta msisimko katika jimbo la kawe. Katika Wilaya ya Kinondoni ambayo ina majimbo mawili ambapo kuna Jimbo la Kinondoni na Jimbo la Kawe kwa ujumla wake zina kata zipo 20, katika kata zote ishirini kata mmoja ndiyo inayoongozwa na Mwanamke yaani Kata ya Mbezi Juu.
Ukienda katika Mkoa Mzima wa Dar Es Saaalma ambao una kata 105, madiwani wa kata wapo 11 ambao ni wanawake. Ni jukumu la TWEA women news kuhakikisha inakutana na kila diwani kwa ajili ya kuandika Makala zao.
Diwani Anna anahistoria kubwa ya kujitafuta kutoka Muuza Duka hadi Diwani! Akiwa amepitia kampuni mbalimbali na baadae kujiajiri kama mtaalam wa masoko, kazi anayoendelea nayo hadi sasa. Kina mama wenzangu inawezekana! Kila kitu ni kuweka malengo. Makala ya Diwani anna naindika kwa ajili ya kuwatia moyo vijana wa Tanzania kwamba ukiwa na malengo safi utafikia ndoto zako tu.
Diwani Anna pamoja na kazi zote hizo yeye ni mama boys! Mama wa watoto watatu wa kiume aliyejitafuta akajipata. Kutoka Kuuza Duka hadi Udiwani. JITAFUTE EWE MWANAMKE shupavu. Ishi
Huyu ndio malkia wa nguvu.
It Can Be Done!
Bi. Fatma Kange pamoja na mambo mengine ni mwandishi wa Makala za wanawake. Ikiwa ungependa kuandikiwa makala yako wasiliana naye kupitia ukurasa huu.
