KAGERA KUTIA FORA KUELEKEA SHEREHE ZA SIKU YA MWANAMKE DUNIANI HAPO KESHO

Mwenyezi Mungu ni Mwaminifu sana

Amtumainiye Mwenyezi Mungu Hafi Maskini.

“Imeandikwa kwamba pepo yako ipo katika nyayo za mama zetu”

Kama unavyofahamu wadau na wananchi wa Mkoa wa Kagera, Nshomiles! Basi mwenyekiti wangu Bi. Leah Gozbert John Mwenyekiti wa Jukwaa la uwezeshaji Wanawake Kiuchumi Mkoani Kagera  alinipigia simu na kunipa taarifa za maandalizi ya Sherehe za Wanawake huko Kagera, nilikuwa na wakati mzuri sana naye. Simu yangu ilija vicheko! Nikicheka huku nikizunguza naye kwa upendo mkubwa!!

Ndugu msomaji wangu, natamani  nitumie zile TONE ya kihaya zile ha ha ha, maana aliniita Madam Fatma Kange, hupenda kuniita hivyo Mwenyekiti huyu wa jukwaa huko Kagera. ………Alisema …….“Nikuambie kabisa sisi tumenunua vitu vya walemavu, unajua wanapata shida sana kwenda  kujisaidia mliwatoni… huku nikimsikiliza kwa makini, nilibaki hee Leah! Maana kwa tone ya Kihaya alafu sherehe za Mwanamke na vyoo vya walemavu  vyenye sink.  Tatizo sio vyoo ni ile TONE na NENO SINK!  Aliongea kwa majigambo.  Ila katika wenyeviti wote wa Majukwaa, Jukwaa la Kagera ni miongoni mwa majukwaa ambayo yako busy sana. Wanafanya vizuri mno!   TUNAJIVUNIA.

“Vilevile tumetengeneza madawati 60” alisisitiza kwamba wanaunga juhudi za Kumsaidia Mheshimiwa Raisi Mama Dkt Samia Suluhu Hassan baada ya kazi kubwa aliyoifanya ya kujenga madarasa. Jukwaa la Kuwezesha Wanawake Kiuchumi  Mkoa wa Kagera limefanya kweli.

Vilevile  katika shule  zenye wanafunzi wenye mahitaji maalum pia wameweza kugawa vifaa vya akina mama wakati wa hedhi, Madaftari, Kalamu na Mafuta ya Kupaka na Sabuni pamoja na Malapa ya kuogea= Yeboyebo

Aliongeza kuwa wamejikita katika kuhakikisha watoto wenye ulemavu wanatengenezewa miguu bandia.

Kagera walishafanya kazi kubwa walizindua majukwaaa karibu mkoa wote.

Hakuishia hapo alinipa siri kubwa ya mafanikio kwamba mambo yote hayo yanafanikiwa kwasababu wana fanya kazi kwa karibu sana na Ofisi ya Mkuu wa Mkoa ambayo inawapa ushirikiano mzuri mno na  wanamfurahia sana Mkuu wa  Mkoa wa Kagera ambaye pia ni wajina wangu Bi. Fatma Mwasa. HONGERENI WANA KAGERA.

Mkoa wa Kagera upo juu

Mkoa wa Kagera umeweza

Hicho ni Kishindo cha Mama.

Mama Dkt Samia Suluhu Hassan Hoyee

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *