Miaka 10 katika Ujasiriamali wa Batiki na Tuzo za Jasiri Awards 2022 na Mhe. Matilda Lugeha. Namuita Mhe kwani nahisi ni Kiongozi katika Tasnia hii ya wanawake na ujasirimali wa Batiki. Wanawake wenzangu napenda kusema hivi, Kujitambua ni dawa! Mwanamke aliyejitambua mahali popote huwa anapata nafasi ya kupenya. Matilda Lugeha ni miongoni mwa wanawake niliokutana nao nchini kwetu hapa ambao, wanafanya vizuri mno.
Matilda ni nani asiyemjua katika kazi za mikono na batiki Tanzania na East Afrika kwa ujumla. Matilda amekuwa ni mshiriki mkuu wa maonesho ya Jua Kali nchini na nchi ya Uganda, Kenya na Burundi. Akizungumzia safari yake ya kuwa mjasiriamali Matilda kama akina mama wengine ana mengi ya kusema na anahitaji majibu ya changamo mpya anazopambana nazo, changamoto ya kukua! Anatamani kufika kuleee! Nimemshauri badili mwalekeo. Ushirika UTAMTOA! Kama mnavyofahamu napigania sana ushirika wa viwanda kwa wanawake na nipo nautangaza nchini na Afrika yote. Ushirika utavusha wanawake wengi.
Mshindi wetu huyu ni mama watoto wa watatu ambaye anajituma sana kusimamia familia, kukimbizana na uchumi pamoja na maisha kwa ujumla akiwa ni mwakilishi wa kundi kubwa nchini linalojihusisha na biashara ya Batiki. Kilichonituvutia ni namna alivyofungua mlango wangu ofsini kwangu leo asubuhi akija kunileta Tuzo yake aliyoipata katika TUZO ZA JASIRI AWARDS zilizotolewa Mkoani Mwanza, 8.05.2022 na Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Mhe Robert Gabriel. Nampongeza mkuu wa mkoa huu kwa kuwapa wanawake TABASAMU.
Alikuwa ni mwenye tabasamu kubwa huku akiingia na kusema madam Asante! Nimejikomboa kupitia hii tuzo nimepata order nyingi. Wengi walioniona kwenye mitandao wananitafuta sasa….!. Nilimpokea na kumtafuta mtu atupige picha mmoja tukae sawa na hili tabasamu kubwa la wanawake nilio wa MENTOR. Kila mwanamke atafute MENTOR wake jamani. Nimeshashauri sana na hapa nasisitiza tafuta MENTOR wako akupange upangike wewe mwanamke msoma Makala zangu. Hebu TUJIONGEZE.
Kikubwa tuzo ya Matilda ina maana gani kwa wanawake wapambanaji? Wachachalikaji au Majembe? Hii ni kwasababu tunamajina mengi sana wanawake tunaojituma. Kila mtu namna anavyokuchukulia. Mara Kiongozi, Jembe, Mpambanaji, mara super woman, yaani majina ni kama yote, binafsi nimechoka kuitwa Mpambanaji. Sasa hiviwananiita Malkia nasema Bora. Bora niwe Malkia kwani nimeshavuka VIKWAZO ha ha ha ha. Jamani niiteni Malkia- nimechoka.
Sasa turudi kwa Matilda wetu, Shuja wangu wa leo ambaye amekuja kunipa Tabasamu la TUZO yake ya JASIRI AWARDS. Alafu kama wewe msomaji unatuzo zako umejifungia nazo, hebu zilete tukutoe na wengine wajifunze kutoka kwako. Au nimekutengeneza kwa njia mmoja au nyingine unatuzo hebu niletee nikupige picha! MATILDA leo kavunja ukimya kaja na tuzo yake jamani, nimefurahi sana. Hebu leteni mituzo hiyo tuwe na furaha zetu na vile Royal Tour ipo katika kutangaza nchi yetu basi tuji Tag huko kwa mambo makubwa naya kimkakati. Hebu tujipromote na Royal Tour yetu, mnataka tupewe nini tena wanawake wazalishaji. Fursa ya kujitangaza ni sasa!.. Leo na mtweet na hashtag ya Royal Tour labda tuzo za Afrika watamuona, Tumuombee, azidi kusonga mbele na ndoto zake zitimie.
Matilda Lugeha anatufundisha kwamba Maisha ni Kuthubutu! Mwanamke yoyote jipange kuthubutu kwa lolote unalopenda kulifanya duniani hakuna aliyekukataza. Yeye alichagua Batiki ingawa kwa upande kiasi anafanya vipodozi vya Asili. Matilda pia anatufundisha kujitambulisha- Kajitambulisha kwa biashara yake ya BATIKI. Nimemuuliza umechukua mdua gani kwenye biashara yako hadi kupata tuzo hii, ana amesema miaka …ni miaka 10 madam…10years Duh! …Mtazame huyu mwanamke… hebu mtafakari…..Kazi kubwa sana kafanya mrembo na Mhe Matilda Lugeha kwa kweli.
Ananiambia kwa furaha tena mtoto wangu wa kwanza akiwa ametimiza miaka 27 na wa mwisho akiwa na miaka 13 na ujasiriamali wa miaka 10 ndio napata TUZO. Asante sana waandaaji wa Tuzo hii Matila alihitaji tuzo! na ndio maana nampongeza Ms Lightness kwa kuandaa Tuzo hizi za wazalishaji kutokea mkoa wa Mwanza na kuweze kumpa tabasamu Mrembo na mpiganaji wetu Matilda Lugeha. Hongera zake na naomba kila mmoja msoma makala yake ampongeze sana kwa hatua alizopinga. AMEWEZA.
Anahitaji msaada zaidi katika kununua madawa na materials za batiki ili aweze kutimiza ndoto zake kubwa. MATILDA anataka kuwa KINARA, Tumuwezeshe. Ofisi yake ipo Chanika na ni miongoni mwa wanawake TWEA ina Tweet wenye hashtag ya =TanzaniaWomenwholead. Kama wewe unafanya vizurikatika jambo lako lolote na ni mwanamke, tafadhali niandikie info@twea.co.tz. Tuyajenge, wapendwa wanawake wenzangu. Wakati ni Huu!.
Wanawake wa Tanzania sasa Kuchelee!
Wanawake wa Afrika walihitaji Ushirika.
