Kama kawaida leo katika andiko langu hili, nazungumzia dhana nzima ya Utafutaji wa Fedha kwa ajili ya Bunifu au Jitihada yeyote uliyonayo. Na kama mnavyojua namlenga mwanamke. Wanawake tunajijua sisi ni watu wa mambo mengi jamani. Tuna mambooooo! Tuko na mambo yetu Lukuki, hebu nicheke kidogo maanake kama movie vile ukimfikiria mwanamke! Kazi kubwa sana! . Ni Silka yetu jamani! ndio tulivyoumbwa asitushangae mtu. Lakini mwanamke ukishajua kwamba wewe una mambo mengi, nakufundisha leo basi chagua mawili tu kati ya hayo toka nayo. Hili nalo ni somo jingine. Leo twende kwenye mada ya namna ya kujipanga kupata fedha kwa ajili ya jitihada yako yoyote uliyonayo.
Leo sizungumizii utafufutaji wa Fedha kwa biashara ndogo ndogo ya mtu mmoja mmoja! Kwani dhumuni langu ni kuwatoa huko. Nazungumizia jitahada ya utafutaji wa fedha kwa kundi kubwa ambao mmeungana na mnataka kutoka. Fedha au mitaji inapatikana vipi? Ndugu zangu, ili kupata fehda kitu kikubwa ni kuwa na mipango. MALENGO. Malengo yatawapa DIRA! Lazima mjue mnapotaka kwenda.
Wekeni malengo ya hilo jambo mnalo amsha! mnalo lianzisha iwe je mnataka kuona nini ndani ya miaka mitano ijayo. Unajua malengo makubwa huchukua muda, sasa mjikusanye mtake mambo makubwa alafu uwaze faida ya ndani ya mwaka mmoja si kichekesho hicho. Mambo makubwa huchukua muda lakini mipango haichukui muda.
Hatua kubwa na muhimu, msijifungie wenyewe kuchakatua hiyo mipango. Hakikisheni mnakuwa na mtaalamu ambaye atawasaidia kupanga mambo yenu. Atawasikiliza na kuwashauri kimkakati. Kupata fedha za mipango mikubwa hata ukaenda kwa benki wanahitaji maandiko. Nia inaweza kuwa nzuri lakini kama haijaandikwa hutopata kitu. Mkishampata mtaalamu hakikisheni anawapitisha kwenye matarajio ambayo mmeshakubaliana na akimaliza mwende naye kwa watoa fedha ili akatetee andiko lenu.
Tunatoa ushauri wa kimkakati katika kusaidia makundi yanayojitambua ili kuweza kushiriki vyema katika kujiletea maendeleo. Neno langu kubwa kwenu “Wanawake wa Afrika wanahitaji Ushirika” Kwa mwenye swali lolote na anayetaka kujifunza zaidi TUANDIKIE TWEA tutakujibu. unaweza kunipigia mmoja kwa mmoja angali mawasiliano kwenye website yetu. www.twea.co.tz
