Wanawake na Agenda Zetu! Fullshangwe!
Mpendwa msomaji wangu wa makala hizi fupi fupi, makala ambazo naona heri niziandike ili zijenge na wengine. Kwa kifupi mfululizo ya makala zangu zaidi uakwenda kwenye ulimwengu wangu wa wanawake! nilioamua tu kuufanyia kazi! Kuutumikia! Ulimwengu wenye hazina kubwa sana katika ulimwengu tunaoishi. Kama kila mwanyamke angejua kuwa yeye ni Malkia angeanza maisha ya kimalkia leo! Unajua kwamba wewe ni malkia? Basi nikianza kumtafakari mwanamke huwa na mfananisha na hadithi ya kusisimua yanye hoja za kisayansi unaotokana na dhana ya “Umalkia wa Nyuki” Laiti kama elimu kidogo ya wanawake ingeelekezwa katika mfano wa Nyuki, tungekuwa na himaya ya wanawake wasiomithilika kwa matokeo makubwa. Jipange kumsoma nyuki na maisha ya nyuki alafu tafuta sifa za Malkia Nyuki uniandikie baada ya kujua thamani ya malkia wa nyuki alafu uje tuyajenge hapa! ha ha ha! -nakupa Home work! Ole wako usinirudishie majibu.
Leo katika makala yangu ndogo, nasema hivi, nimekuwa na simu nyingi wakina mama wengi wakitaka niwatengeneze! Jamani asanteni kwa wale wote mnaohudhuiria masomo yangu yangu ninayoyatoa kama ” Mafunzo ya Uongozi wa Taasisi Zinazoendeshwa na Wanake”. Personal Development Training, Elimu ya Ushiririka kwa viwanda vya Wanawake, vilevile na Interivew zangu ambazo zote zimejikita katika ulimwengu wa wanawake. Ukiona unahitaji kukarabatiwa katika maeneo hayo karibu sana. Wewe niandikie tu hakuna shida.
Leo nimeguswa niwaambie jambo, yaani wewe mwanamke kama unataka UJITOKEZE- Extend katika mambo yako na kujitambue huku ukiishi ndoto zako, kubali kabisa kwamba ipo kazi ya kufanya. Kwanza ni kutathimini hatua uliyofikia, iangalie kama unaridhika nayo alafu ndio uje na mikakati wako! NTAKUONGOZA.
KUTOKELEZEA ni kujipanga katika mbinu za kutimiza yale malengo ambayo ungependa kuyafikia. Ikiwa unaamini kwamba, huna kosa au hujakosea kiufundi katika stage ya maisha uliyofikia, kamwe hutoweza kubadilika. Kuna kitu kinaitwa Evaluation- hii ina maana ya kujikagua kwa kulinganisha thamani ya wakati na matokeo uliyokuwa nayo je yanaendana na mipango uliojiwekea? au, yapo kinyume? Ushakuwa na mipango best? au vile unaenda bora liende? KATAA!
Basi chukua kalamu yako na karatasi na nipe malengo yako na ukiona unahitaji maoni zaidi au kujiandikisha katika masomo yangu yajayo nitumie message tuyajenge.
Wanawake wa Tanzania sasa kuchelee!
