Leo nimeona kidogo kama nimechokoza kwenye ukurasa wangu wa Instagram Juu ya nafasi ya Royal Tour na wanawake wa Tanzania. Mhe Raisi mama Samia Suluhu Hassan kafanya jambo kubwa sana nchini na Duniani kwa ujumla wake. Katutengenezea jambo ambalo kwa wenye macho hawaambiwi Tazama. Kikubwa nimejipa nafasi ya kuwajengea uwezo wanaweke wa Tanzania waliopo kwenye biashara, Ujasiriamali na Viwanda juu ya mambo mengi muhimu hasa taarifa za kibiashara na viwanda kwa ajili ya ustawi wao kwa ujumla, kwa njia ya kuwapa taarifa kwa lugha rahisi/ nyepesi ili waweze kuchukua fursa. Ikuchukuliwa kwamba wanawake wengi ndio wazalishaji mali hapa nchini. Lugha nitanayotumia katika makala zangu itakuwa ni rugha rafiki na rahisi.
Leo ningependa sana kuizungumzia “Royal Tour Tanzania”. Naizungumzia kwa sababu ningependa sana kuihusisha na nafasi ya mwanamke katika uchumi , biashara na usawi wa jamii. Mfano nitaonyesha mifano michache sana swali je “Royal Tour” itamsaidiaje mwanake wa kawaida hasa wa hapa kwetu Tanzania katika kujipanga kimkakati? Yaani kuchukua fursa na kuzitumia.
Dunia yote ni ya wafanya biashara! Biashara zipo katika maeneo mbalimbali na kila nchi inazungumza lugha kulingana na uchumi wa nchi yake unavyoipeleka. Zipo nchi tunazoziita zimeendelea na hizi za kwetu zinazoendele, Nchi hizi hutofautiana kimkamakti katika kujenga mambo yao. Kikubwa tunatakiwa kujua kwamba, maisha ya binadamu yamejikita zaidi katika kuzalisha na kutumia . Katika kutumia wapo wale wanaozalisha na wale wanao nunua! Huu ndio uchumi na hii ndio biashara. Tanzania ni nchi ambayo ilipanga kuwa nchi ya uchumi wa kati hadi ifikapo mwaka 2025. Hii ndio ndoto kubwa ya nchi yetu, ambapo sasa tunapokimbizana na ndoto hiyo ni lazima yalaziliwe mambo makubwa, kwa muono wanangu! Mijimambo hiyo mikubwa sisi wanawake wa Tanzania tusiishie kuipigia makofi ni lazima ifike mahali tujiulize au tujipange nayo kwamba, je tunawezaje kunufaika na hatua za kusisimua zinazopigwa katika nchi hii yetu hii ya neema? Mkiangali huku na huko mara kuna miji miradi mingine kama mi-SGR, mara Mibarabara mikubwa inayojengwa, mara maumeme yanatandikwa tena ya kisasa! mijedege inapaa juu tena ya kushangaza! Kikubwa nanyie wanawake mkazipande sasa! Cha kufurahisha na kuona inabidi tujipange tena kimkakati na kisawasa ni kuchukua fursa. Mambo makubwa ni mengi kiasi ambacho kabla hamjajipanga linakuja jingine la Royal Tour kubwa mno nala kupendeza kwa lugha ingine yaani hatupoi! mijimambo mingi mingi tena mizuri sana kwa ajili yetu. Kazi Zinaendelea.. Asante sana mama.
Kwa kifupi ninachoona kazi kubwa ni kwa wanawake kukaa na kuchukua hatua na kuona namna mambo yote yanayoendelea na yanavyoweza kutujenga zaidi kimkakati. Ndio maana leo katika kuitafakari “Royal Tour” nimeona niwaambie kwamba msimu huu wa “Royal Tour” una maana gani kwa wanawake wachacharikaji, wakandarasi na wafanyabiashara, Ma Super Women, Wapiganaji na wajasiriamali kwa ujumla?- Infact wanawake wanaothubuti nchi hii wanamajina lukuki.
Wanawake Royal Tour maana yake ni Branding! hivi mnajua maana ya neno “branding” …….. labda …..nitumie Lugha rahisi hapa, Branding ina maana kwamba- Royal Tour na kujitambulisha! …….Taifa letu Linatambulishwa jamani! ……nafikiri naeleweka “Branding” ni Chapa! Chapa kuona na kuielewa! Hivyo kwa lugha rahisi Tanzania yetu kwa sasa ipo katika Utambulisho mkubwa wa kimkakati ulimwengu kote kama sio Duniani kwa ujumla! Huu utambulisho una maana gani kwako mwanamke mchacharikaji? Hii ndio hasa imenisukuma kuandika hii makala ndogo tu kwa namna Mwenyezi Mungu alivyonijalia nami nitoe mchango wangu na kupongeza jitihada hizi nzuri zenye sura ya kuvutia zinazoendelea hapa nchini chini ya Mama yetu mpenzi Mhe Raisi. Utambulisho wa nchi yetu mama anafanya kazi kubwa mno!…. Hivyo jamani kazi inabakia kwako! JIPANGE MWANAMKE! AMKA! Chukua fursa ya kujitangaza kupitia Royal Tour. Kwa mfano tunataka mama afanya nini zaidi? Amkeni wanawake wenzangu na dandieni fursa hii kubwa na nitawaambia kwanini. Huu ni utambulisho wa bure ambao unaibeba Tanzania na kila kilichomo kukitangaza! sasa wewe mwanamke lazima ujue kwamba upo kwenye kipindi cha neema ya ajabu.
USHAURI WANGU- Wanawake wenzangu watafutaji , utambulisho unaobeba nchi yetu wa Royal Tour utahitaji mwanamke aliyejipanga vizuri. Anzisha basi ka Social Media kako ambako unatangaza vitu vyako ingiza na hashtag ya Royal Tour kukutangazia biashara yako. Jizatiti kwa utambulisho wa kimkakati katika mitandao ili uweze kutumia fursa hii kubwa ya kuitangaza nchi inayoendelea huku biashara yako ikitangazika, kupitia hii fursa ya pekee nchini na duniani kote. Kwa mfano kwa sasa Unaweza kushiriki mikutano mbalimbali ya kimtandao inayoendana na biashara yako huku ukijinasibu kwamba wewe ni mtanzania ambaye mnazunguka nchi mbalimbali duniani kutanganza Royal Tour. zaidi ya hapo matangazo ya jambo hili yanayokwenda mkoa kwa mkoa ni fursa kubwa pia. Tuitumie.
USHAURI MWANGINE-Tafuta wabia kupitia jitihada mbalimbali za nchi yetu ili wawekezaji wakija waweze kuwekeza katika biashara zako kwani sasa hivi ni dhahiri watu wengi hasa wawekezaji watahitaji wabia wa kitanzania kwani mazingira ya uwekezaji ni rafiki . Kuwa tayari na kaa kikazi zaidi, na ili kupata wawekezaji unaweza tembelea taasisi kama CTI, TIC na TANTRADE kuulizia juu ya mambo hayo ya uwekezaji na kujipatia taarifa lukuki. Wakati ni huu akina mama. Tuchangamke! na TUJIPANGE zaidi.
Napenda kuwakumbusha tu kwamba jamani Royal Tour ni Nguzo kubwa sana ambayo mama ameisimamisha hapa nchini na Duniani kote na ni wajibu wetu kuishikilia ili izidi kutupandisha mwisho wa siku tutasherekea matunda ya kazi hiyo adhimu hapa nchini kuwahi kutokea. Mama anavyoupiga mwingi tufunge kibwebwe tucheze naye ngoma, kwani kuna msemo usemao Ukibebwa jilegeze! Tutajilegeza kwa kutafsiri thamani ya jambo hili la Royal Tour kwa kuchukua FURSA.
Mungu ibariki Tanzania, Awabariki Viongozi wetu wote na Bariki Wanawake wa Tanzania. Royal Tour inatuhusu saana wanawake.
Wanawake Tanzania sasa kuchelee.
Wanawake wa Afrika walihitaji Ushirika
