Tume ya Maendeleo ya Ushirika nchini (TCDC) chini ya Uongozi wa Mrajisi wa Tume, Ndugu Dr Benson Ndiege kwa mwaka wa pili mfululizo umekuwa ukiandaa Kongamano la Utafiti juu ya maendeleo mbalimbali ya ushirika nchini. Kongamano hilo hutumika kama sehemu ya kutoa mrejesho ya mafaniko mbalimbali yanayopatikana katika kujenga ushirika nchini Tanzania. Vyama vyote vya ushirika hushiriki katika kongamano hilo pamoja na maafisa ushirika.
Mwaka huu chama cha Ushirika wa Viwanda vya Wanawake nchini, kinachojulikana kama MADIRISHA Women Cooperative Society kimeshiriki katika kongamano hilo kama sehemu ya kujitambulisha rasmi kwa umma wa Ushirika nchini. Chama hiki, maelengo yake makubwa ni kuhamasisha wanawake kuzalisha kupitia mfumo wa Ushirika kwa vitendo. Malengo yake ni makubwa na kinazidi kujipanga.
Viongozi kadhaa wa bodi pamoja na baadhi ya wanachama wa ushirika wa wanawake wa MADIRISHA wameshiriki katika kongamano hilo kubwa na muhimu kwa maendeleo ya ushirika nchini. Tume ya maendeleo ya ushirika inafanya kazi kwa karibu na chama hiki ambacho kimeamua kujitambulisha kwa umma juu ya nia yao ya kufanya uchumi wa ushirika kwa wanawake nchini.
Kupitia kongamano hilo chama cha ushirika wa viwanda vya wanawake nchini, kinatumia jukwaa hilo kama sehemu ya kujifunza na kujitambulisha kwenye vyama mbalimbali vya ushirika vinavyoshiriki katika kongamano hilo. Taarifa maalumu inategemewa kutolewa rasmi kutoka kwa Afisa habari wa Madirisha Bi Anna Mary Leone Kavishe.
Kazi ya Tume ya Ushirika ni ya kupongezwa na MADIRISHA wameshukuru kuhusishwa.
Wanawake wa Afrika wanahitaji Ushirika.
Wanawake wa Tanzania sasa Kucheleee!
