SIMULIZI ZA LUKUNDO

KITABU CHA SIMULIZI ZA LUKUNDO KINAPATIKANA SASA

Kitabu murua kwa ajili ya watu kujisomea cha simulizi za lukundo sasa kinapatika kwa njia ya bei ya jumla na rejareja. Kitabu hiki kinapatika katika ofisi za TWEA zilizopo Kunduchi Beach, Mtaa wa Kilongawima Nyumba na 93.

Kitabu cha Simulizi za Lukundo ni kitabu kilishojitambulisha kama kitabu cha kiafrika chenye nia ya kuonesha neema mbalimbali za makuzi yetu ambayo yanafanya mwafrika awe na thamani kubwa duniani. Kinatupitisha kuiona thamani ya mwafrika kwa kumzungumzia Bibi Kozaina akitumika kama kinara katika kujenga picha kubwa ya mambo ya kikwetu kwetu! ya kiafrika ambayo watu wengi huyachukulia poa.

Uafrika ni umarididi na umashuhuri. soma kitabu hiki na chungulia mzunguko wa maisha ya Bibi Kozaina na uione bahati ya kua mwafrika.

Katika ukurasa wangu wa Youtube- Nazungumzia kwanini niliandika hiki kitabu! Fuatilia makala hizo ili uweze kujifunza mengi https://www.youtube.com/watch?v=tyPyM1udhrk&t=3s

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *