KUTANA NA ENG. LILIAN MWANGOKA MSTAAFU WA TCRA ALIYEAMUA KUSIMIMA WANAWAKE WA VIWANDA VYA USHIRIKA KUPITIA USHIRIKA WA VIWANDA VYA WANAWAKE VYA VINAVYOFUATA DHANA YA MADIRISHA.

Mwenye Mungu ni Mkarimu

Hutenda kwa wakati wake .

KUTANA NA ENG. LILIAN MWANGOKA MSTAAFU WA TCRA ALIYEAMUA KUSIMAMIA WANAWAKE NA VIWANDA KUPITIA USHIRIKA WA VIWANDA VYA MADIRISHA.

Eng. Lilian Mwangoka ni mstaafu wa TCRA ambaye ametumikia eneo lake la kazi kwa muda mrefu  kwa zaidi ya  miaka 30 ambaye amelitumikia Tiafa kwa upendo uliotukuka akianza kazi zake baada ya kufuzu mafunzo yake kutoka Chuo Kikuu Cha Dar ES salaam enzi hizo. Lilian ndio kati ya wanawake wa chache wa kwanza kwanza wa nchi yetu waliobebea katika masomo ya science. Baada ya kumaliza chuo kikuu miaka hiyo aliajiriwa na eneo lake la kwanza kufanya kazi ni ndani ya Jeshi la Polisi. Yeye ni mtaalam wa kurusha mitambo na kusimamia  mifumo ya mawasiliano kwa njia ya masafa. Alipo malizia  ajira yake hiyo baade alijiunga na Kampuni ya simu Tanzania ambapo alifanya kazi kwa miaka 9. Mabadiliko na namna sekta ya mawasiliano ilivyozidi kukua ndipo baada ya kuanzishwa aliweza tena  kuingia katika mamlaka ya mawasiliano  kwa ambapo alifanya kazi kwa miaka kumi na sita 16

Eng Lilian Mwangoka baada ya kustaafu kwazi kwake mwaka 2022 alijiunga na Ushirika wa Viwanda vya Wanawake vya MADIRISHA uliojipanga. Ushirika huu umeamua kuisimamisha SACCOs yake ambayo imeanza kutoa mikopo kwa wanachama wake.

Katika ushirika huu, lengo ni kuusambaza ushirika huu kwa wanawake katika ngazi mbalimbali za kiuchumi ili uweze kuwasaidia kujiongezea kipato.

Katika harakati za kuhakikisha wanawake wengi wanajifunza na   kujiongezea kipato chao, chama cha ushirika wa viwanda kwa mara ya kwanza kilianzishwa mwaka 2020 kwa lengo ya kuingiza viwanda vya wanawake kwenye  ushirika yaani Tanzanai kuwa na Cooperative Enterprises.

Eng Lilian Mwangoka,  atakuwa msaada  mkubwa kwa ushirika huu kwani,  analeta  uzoefu wake wa utendaji wa serikalini katika kuwasaidi wanawake walioamua kujitafuta hapa nchini.

Amepokelewa na bodi ya Madirisha Women Cooperative Society  kwa moyo mkunjufu tukisubiri ajenge na kuratibu masuala ya ushirika wa viwanda kimkakati.

Kwa wanaohitaji kupata mikopo na kuwa wanachama wa MADIRISHA SACCOs wasiliana na Mhamasishaji wa masuala ya ushirika huu Bi Annamary Kavishe

Hongera Eng Lilian Mwangoka

Karibu Madirisha.

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *